*JESHI LA POLISI TOENI ELIMU KWA ASKARI WENU MAANA MNACHAFULIWA NA WACHACHE WASIOJUA MAADILI YA ASKARI.
---
SI MARA YA KWANZA KWA WAANDISHI KUKUTWA NA HILI. NA NINAAMINI NI ASKARI WACHACHE KATIKA JESHI LA POLISI WASIOJUA WAJIBU WAO.

NIMEZALIWA KWENYE KAMBI YA JESHI MZEE WANGU ALIKUWA ASKARI POLISI NA NIKALIPENDA SANA JESHI LA POLISI NA SIKUONA HAYA YA ASKARI KUPIGA MWANDISHI LAKINI KWA SASA YAMEZIDI KIASI KWAMBA INATENGENEZA UADUI KWA WATU WANAOTEGEMEANA KATIKA KUFANYA KAZI.

SITASAHAU SIKU YA JANA AGOSTI 8, 2018 UWANJA WA TAIFA, JIJINI DAR ES SALAAM UMESIMAMA UNAPIGWA, UMEKAA CHINI UMEPIGWA, UMELALA UMEPIGWA SASA SIJUI WALITAKA NIPIGANE NAO HALAFU KISA NINI HATUTAKIWI KUINGIA KWENYE PRESS CONFERENCE WAKATI TUMEVAA NA KITAMBULISHO. KWANI MKIONGEA AMUELEWEKI HADI MPIGE? AU KAMA KUNA HATARI YA USALAMA KUNA ONYO LOLOTE MLITOA?

SHUKRANI KWA WAANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO WALIOPIGANIA KUMSIMAMISHA NA KUONGEA NA WAZIRI LUGOLA NAYE KUAMURU NITOLEWE WAKATI HUO NIKIWA KWENYE KARANDINGA USO UMEUMUKA.

SHUKURANI @tanfootball PAMOJA NA TASWA KWA KULIONA HILI INGAWA KWA KUCHELEWA NATUMAINI HALITATOKEA TENA.

JESHI LA POLISI TOENI ELIMU KWA ASKARI WENU MAANA MNACHAFULIWA NA WACHACHE WASIOJUA MAADILI YA ASKARI.

SILAS MBISE.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: