Hali ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Hamis Kigwangalla yazidi kuimarika ambapo jana Agosti 13, 2018 aliweza kufanya mazoezi ya kupanda ngazi kwa miguu kutoka ghorofa ya kwanza hadi ghorofa ya sita katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikolazwa ikiwa ni siku ya 14 sasa tangu alipopata ajali ya gari mkoani Manyara.

Waziri Kigwangalla amesema hayo leo Agosti 14, 2018 wakati Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga alipomtembelea katika hospitali hiyo kwa ajili ya kumjulia hali na kumpa pole.

"Namshukuru Mungu hali yangu inazidi kuimarika jana nimefanya mazoezi nimetoka hapa nimekwenda hadi chuoni kwangu niliko soma na kurudi" alisema Waziri Kigwangalla
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: