Tamasha kubwa na la aina yake la muziki wa Kiafrika ambalo ni maalum kumuenzi gwiji wa muziki Hayati Dk. Remmy Ongala lililopewa jina la ONGALA MUSIC FESTIVAL, linatarajia kulindima kwa mara ya kwanza katika fukwe mwanana za Malaika Beach Club, Kigamboni.

Akizungumza Mratibu wa tamasha hilo Bi. Aziza Ongola anaesimamia mfuko wa Ongala (Ongala Foundation), amesema tayari maandalizi yote yameenda vizuri na watu wakae mkao wa kulishuhudia tamsha hilo ambalo ni la urithi wa muziki kutoka kwa gwigi Dk. Remmy.

Aziza amesema kuwa, Wasanii mbalimbali kutoka Nchi tofauti za Afrika na bendi zao watatoa burudani kwa muda wa siku tatu yaani kuanzia Agosti 23-25,2018 katika fukwe hizo za Malaika, Kigamboni.

“Tutamuenzi Baba kupitia nyimbo zake nyingi ambazo zimekuwa na umaarufu ndani na nje ya Afrika. Hivyo tamasha ili ni kuamsha hali ya Muziki aliouacha na pia kuendelea kumkumbuka kupitia mashairi yake” alieleza Aziza.

Aziza ameongeza kuwa, tamasha hilo pia litasaidia kuimarisha kumbukumbu na kazi za gwiji huyo aliyefariki Desemba 2010, Nchini.

Kwenye tamasha hilo vikundi 22 kutoka nchi mbalimbali za Afrika vitatumbuiza kwa siku hizo tatu.

Miongoni mwa wasanii hao ni msafiri Zawose, Ally Swahi, Siti and the Bend, Hokororo, King kiki na Sikinde. Pia atakuwepo Ashimba, Carola Kinasha na wengine wengi

Pamaoja na buradani hizo zitakazoanza muda wa jioni, pia milango itafunguliwa kuanzia asubuhi kwa Semina na Warsha kwa wasanii, Biashara mbalimbali na micheze ya Watoto.

Kiingilio kwenye tamasha hilo ni Tsh. 10,000/ kwa mtu Mmoja huku gharama hiyo ya kiingilio ikitarajiwa kupungua kwa kuanzia watu watano gharama zitapungua.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: