Watumiaji wa bia ya Castle wakipiga picha wakati wa promosheni eneo la Boko.
Kata mti panda mti ikiendelea wakati huo huo wadau wakipiga picha kwa pozi mbalimbali.
Maofisa Waandamizi wa Masoko wa TBL ndani ya promosheni hiyo.
Mambo ya Unlock na Castle yakiendelea.
Vijana hawakubaki nyuma katika ku unlock na Castle Lite.
Ni mambo ya Castle Lite kwenda mbele.

Kampuni ya TBL kupitia bia yake ya Castle Lite, imezindua promosheni kubwa ya wiki 13 inayojulikana kama Unlock Castle Lite, kwa lengo la kuleta burudani kwa wateja wake katika mabaa mbalimbali yaliyopo katika wilaya zote za jiji la Dar es Salaam.

Lengo kubwa la promosheni hiyo ni Kutangaza chapa na kuwashukuru wateja kwa kuendelea kufurahia EXTRA COLD CASTLE LITE!.

Tofauti na promosheni zilizozoeleka ,promosheni hii imesheheni kila aina ya burudani ambapo inaweza kuwakutanisha ndugu ,jamaa na marafiki pamoja na kupiga picha mbalimbali huku wakifurahia kinywaji bia ya Castle Lite.

Unlock Castle Lite,ambayo inafanyika katika siku za Alhamisi na Ijumaa baada ya saa za kazi pia inawashirikisha wafanyakazi wa kampuni ya TBL ambao wanajumika pamoja na wateja na kuwapatia zawadi mbalimbali za promosheni.Tayari wakazi wa Kawe,Boko na Tegeta wamefikiwa na Unlock Castle Lite.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: