NAIBU Waziri wa Madini Dotto Biteko akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja ya kutembelea Hifadhi ya Amani kulia ni Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo.
NAIBU Waziri wa Madini Dotto Biteko akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja ya kutembelea Hifadhi ya Amani.
NAIBU Waziri wa Madini Dotto Biteko kushoto akimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja ya kutembelea Hifadhi ya Amani.
NAIBU Waziri wa Madini Dotto Biteko kulia akimsikiliza kwa umakini Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu wakati wa ziara yake ya siku moja.
NAIBU Waziri wa Madini Dotto Biteko kulia akiwa na Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu na Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo wakati wa ziara yake ya siku moja wilayanu humo.
MBUNGE wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu kulia akisistiza jambo wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Madini Dotto Biteko kushoto katikati ni Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo.
Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu akizungumza na wananchi wa kijiji cha Sakale katika kata Mbomole Tarafa ya Amani wilayani Muheza wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Madini Dotto Biteko juzi kulia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza, Mhandisi Mwanasha Tumbo.

SERIKALI imesema kuwa itafanya mchakato wa kuleta wataalamu wa utafiti wa miamba (GST),maliasili na mazingira kwa pamoja katika kata ya Mbomole tarafa ya Amani ili kuweza kuona uwezekano wa kuwaruhusu wananchi na wachimbaji wadogowadogo kuchimba madini katika eneo hilo.

Hayo yamesemwa na Naibu waziri wa Madini Dotto Biteko alipotembelea katika kijiji cha Sakale katika kata hiyo wakati akizungumza na wananchi waliomuelezea kero yao ya kuzuiwa na serikali kutokuchimba madini eneo hilo licha ya kuwatokuwepo na viashiria vya uharibifu wa mazingira na misitu kama serikali inavyosema.

Wakizungumza kijijini hapo wananchi hao walimueleza naibu waziri huyo kuwa madini katika eneo hilo yaligunduliwa mwaka 2013 na ni mengi yanapatikana kwenye miamba na siyo kwenye chanzo cha mto kama serikali inavyosema lakini walizuiwa kwa tahadhari ya uharibifu wa mazingira na misitu ya asili.

Walisema kuwa kutoka uliopo mwamba unaosadikiwa kuwa na madini na chanzo cha maji ni zaidi ya mita sitini na ilipo hifadhi ya msitu wa asili wa Amani ni zaidi ya mita 3,000 lakini wamekuwa wavumilivu kusubiri hatima ya serikali.

“Mheshimiwa naibu waziri uchumi tunao lakini tunakufa maskini…hapa madini yapo lakini serikali imetuzuia kwa hatari ya uharibifu wa mazingira ..sisi tunakuhakikishia hakuna uharibifu wowote wa mazingira utakaotokea” alisema Shetwai.

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Muheza balozi Adadi Rajabu alimuomba naibu waziri Biteko kuleta wataalamu wa madini kuja kupima ili kuona kama madini hayo yanatoka milimani au yapo kwenye mto ili kuona namna ya kuwasaidia kupewa eneo la uchimbaji.

“Mheshimiwa naibu waziri pale mwamba uko pembeni kutoka chanzo cha maji na wananchi wa Sakale kata ya Mbomole wametunza msitu wa asili wa Amani….hivyo wakipewa eneo la uchimbaji wataweza kutunza msitu bila ya kuathiri chanzo cha maji” alisema.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: