Bodi ya Wadhamini ya Hifadhi ya Taifa Tanzania (TANAPA) imeidhinisha na kuruhusu matumizi  ya bajeti ya mpito ya kiasi cha shilingi 3.9 bilioni zitumike kwa ajili ya  kuimarisha uhifadhi, uendelezaji utalii pamoja na ujenzi wa miundombinu katika Mapori ya Akiba matano yaliyopandishwa hadhi na kuwa Hifadhi za Taifa.

Hatua hiyo imekuja kufuatia tangazo la Serikali la kuyapandisha  hadhi Mapori ya Akiba ya Bihalamulo,Burigi, Kimisi, Ibanda na Rumanyika kuwa Hifadhi za Taifa  kupitia kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Hamisi Kigwangalla  alipotangaza Bungeni  wakati alipokuwa akihitimisha  bajeti ya Wizara mwezi Mei  mwaka huu mjini Dodoma.
Ofisa Mwenye Wadhifa wa Mkuu wa Hifadhi, Damian Saru amesema hayo   mbele ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga  wakati alipotembelea  mapori hayo ikiwa ni  ziara yake ya   kikazi ya siku tatu mkoani Kagera kwa ajili ya kufuatilia hatua za uendelezaji zilizofikiwa na TANAPA katika  mapori hayo.

Kwa upande wake, Naibu Waziri , Mhe.Hasunga amesema ameridhishwa na hatua nzuri iliyofikiwa na TANAPA katika mapori hayo na pia ameupongeza ushirikiano kati ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania ( TAWA) na TANAPA katika hatua ya kutoka kwenye Mapori Akiba na kuwa Hifadhi za Taifa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: