Makamu Mkuu wa Chuo anasikitika kutangaza kifo cha Profesa Emil Namakuka Kikwilu kilichotokea usiku wa tarehe 27/08/2018 maeneo ya Kimara, Dar es Salaam.

Prof. Kikwilu ametumikia Chuo katika nyadhifa mbalimbali kama Mkuu wa Skuli ya Afya ya Kinywa na Meno mwaka 1991 – 1997 na mwaka 2006 – 2009 na pia kama Naibu Mrajisi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Sayansi za Afya Muhimbili mwaka 2002 - 2003. Kabla ya kifo chake marehemu Emil N. Kikwilu alikuwa Profesa katika Idara ya Afya ya Kinywa na Meno kwa Watoto na Jamii (Department of Orthodontics, Paedodontics and Community Dentistry) katika Skuli ya Afya ya Kinywa na Meno.

Mwili wa marehemu Prof. Kikwilu utaagwa na wanajumuia wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi siku ya Alhamisi tarehe 29 Agosti 2018, kuanzia saa nane kamili mchana katika eneo la Chuo kampasi ya Muhimbili. Marehemu anatarajiwa kuzikwa siku ya Ijumaa tarehe 31 Agosti 2018, Kimara mwisho.

Makamu Mkuu wa Chuo pamoja na jumuiya ya MUHAS wanaungana na familia ya marehemu Emil N. Kikwilu katika kuomboleza msiba huu.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina

IMETOLEWA NA:
OFISI YA HABARI NA MAWASILIANO YA UMMA - MUHAS
29/08/2018
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: