Juzi nilivutwa na ujumbe wa Mhe. Waziri January Makamba aloubandika kwenye kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Ujumbe ule ukiwalenga wateule wapya wa Mh. Rais Dr. J.P.J. Magufuli akiwaasa baadhi ya mambo ya kuepuka "the don'ts" kwenye nafasi hizo mpya za utumishi wenye mamlaka.

"Usikubali mtu akakubebea mkoba"

"Usikubali mtu akakupakulia chakula kama mnakula kwenye bufee"

Ingawa naweza kuwa sijanukuu kwa usahihi wake, hayo mawili ni baadhi ya mambo aliyoandika waziri Makamba akiwaambia wateule hao ambao katika andiko lake aliwaita "wadogo zangu"

Ni jambo la kupendeza haswaa kunapotokea mtu mzoefu kwenye nafasi za uteuzi kutumia muda wake kuwakumbusha wateule wapya mambo madogomadogo kama hayo ambayo kimsingi huwa ni kero ambayo mtu hawezi kusema.

Binadamu tumeumbwa na akili za ajabu sasa, nadhani mtu anapokuwa kiongozi kuna mambo anakosa fursa ya kuyaona kuwa si mema.

Na kwa kuwa ni kiongozi tayari na anamamlaka ya uongozi huo, nadhani pia hukosa fursa nyingine ya kumpata mtu wa kawaida wa kumwambia hiki hakiko sawa.

Bahati mbaya kabisa aliyonayo mtu mwenye madaraka ni kuwa, wengi kati ya wale anaotembea nao kila siku na kufanya nao kazi hupenda kuheshim fikra na matendo ya kiongozi hata pale fikra hizo zinapokuwa na mkanganyiko, na matendo yake yanapokuwa ya ajabu watu hao humkubalia tu....ndiyo boss.....ndiyo mheshimiwa.

Matokeo yake viongozi wengi hujikuta wananafikiwa weeee ilihali wakiamini kila kitu kiko sawa. Wanapangwa sana.

Zimbabwe alikuwepo mama mmoja mke wa Rais Robert Mugabe. Nadhani anaitwa Grace Mugabe. Mwanamama huyo alitaka haswa kuwa mridhi wa Mugabe.

Akawakamata vijana wa chama kikuu nchini humo. Kimsingi alikwisha kuwa na mamlaka makubwa tu.

Mtu pekee aliyemwona angemnyima fursa ya kurithi mikoba ya mzee ni Rais wa sasa wa nchi hiyo Emanuel Mnagangwa.

Mama yule akiwa kwenye mikutano alimtolea si lugha chafu bali matusi. Siku chache kabla ya Mugabe kufurushwa madarakani alinukuliwa akisema.

Munagangwa alikuwa nyoka alostahili kupigwa tena sio kupigwa hovyohovyo bali kupondwa pondwa kichwa.

Maneno yale yakaonekana ndiyo yanafaa zaidi. Yakashangiliwa na vijana, yakanukuliwa na vyombo vya Habari nchini humo. Mwanamama akapewa sifa kwa hotuba yenye mvuto.

Kumbe ukweli ukijulikana ila haukusemwa kwa sababu walopaswa kusema ukweli waliogopa mamlaka ya Grace.

Hongera January viongozi msijinyime fursa ya kujua ukweli #mnapangwa_sana_aisee.

Ray Mtani.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: