Binadamu wote ni wazuri, ila uzuri unatofautiana viwango, na Mungu alituumba tofauti kwa sababu yeye atukuzwe, na pia anayo sababu ya kumuumba kila mwanamke jinsi alivyo.

Usiingie kwenye ndoa kwa kutazama uzuri wako wa nje, utakupoteza. maana tumeona wazuri wa nje ambao ni wazuri kweli kweli ila bado wanapewa talaka.

Usifikiri utaolewa na mtu mkubwa sana kwa sababu ya uzuri wako wa nje, utapotea.

Usikimbilie kupamba uzuri wako wa nje ili upendwe, usiangalie ulivyoumbika ukapata kiburi, ukajiona hakuna kama wewe, ukaona wengine sio wa viwango vyako. utapotea.

Usitumie uzuri wako wa nje, kufanya mambo ambayo ni kinyume na mapenzi ya Mungu, kama ulikwisha fanya hivyo, basi badilika anza upya.

Wekeza nguvu kubwa kupamba utu wako wa ndani, uwe mwanamke mwema,

Mith 31:30 UPENDELEO HUDANGANYA, UZURI NI UBATILI, BALI MWANAMKE AMCHAYE BWANA NDIYE ATAKAYESIFIWA.

Kumcha Bwana ni kutenda mema. Uzuri wa nje unaharibika wakati wowote, unaweza pata ajali sura yote ikaisha, unaweza ugua uzuri wote ukapukutika, jiulize Ukifa leo, wangapi watakulilia kama mama yao, kama msaada wao, kama mshauri wao, kama msaidizi wao, wangapi?
biashara yako ikifa nani atalia kwa Mungu akuinue tena? Matendo ya mitume 9:36 Dorcas alikufa, lakini akina mama walilia mpaka dorcasi akafufuliwa na Petro kwa maana walikua na cha kumlilia, alikua akitoa sadaka, aliwashonea nguo nk.

Wewe ukifa utaliliwa kwa kipi?.

Yule mwanamke mshunami, mwanae alifufuliwa mana alikua ametoa sadaka yake mbele za Bwana, alikua akimlisha nabii, na kumpa mahali pa kulala.

Kama mwanamke acha maringo, acha kujisikia, acha kujiona wewe bora wengine hawafai, acha kupambana na utu wa nje mpaka unamsahau Mungu, tenda mema.

Kila mtu atahukumiwa kwa matendo yake mbele za Mungu. sio kwa utu wa nje. Huu utu wa nje ni Box tuuu, litarudi udongoni, utu wako wa ndani ndio utakoishi milele.
EZEKIELI 16:15
EZEKIELI 15:25
Umetumia uzuri wako kufanya machukizo mbele za Mungu sasa basi. Hakuna anayeomba toba asisamehewe, labda kama umemkufuru Roho mtakatifu tu, ila hayo yote uliyofanya kinyume na mapenzi ya Mungu omba toba na rehema, anza upyaaaa. Mungu anakupenda sanaaa,

Ukitenda wema, hauozi. utakumbukwa milele.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: