Na Samuel Nathaniel Sasali

Raha Ya Social Media, hakuna ambaye ana maisha mabaya kila mmoja yuko vizuri, huku hakunaga Wabaya na Wasio Ma handsome, huku Social Media hakuna asiye na akili kila mmoja ni mwandishi, Mshauri na mjuzi wa mambo mengi. 

Huku social media hata wanaopitia nyakati ngumu wanaandika maneno ambayo yanawaonesha wao ni Imara kama Simba, Ukikutana na Walioachwa na Wapenzi wao humu Social Media maneno yao yalivyo na nguvu utatamani na Wewe uachwe uthibitishe unaweza ishi bila mpenzi. 

Kuna watu wana post hela wameshika wanavyozihesabu na kumshukuru Mungu amewaonekania haki ya nani tena utajiona wewe ni bwege mtozeni sababu una madeni mpaka vicoba wakati mwenzako kila siku ana post midola na elfu kumi kumi anaandika "another miracle". Ndugu yangu usijione wewe ndo una nuksi duniani sababu na wewe unahamu ya Kupost Ulingishie. 

Usipate tabu tunafahamiana sana sie watanzania ingawa sio wote lakini wengine wana hali mbaya sana kuliko wewe usiye Post. Kuna watu wanaombaga hadi "Location" kwa ndugu zao paonekane kwake, kuna wanaoazima hela za Wajomba zao kututishia nyau, kuna wengine wako Morogoro kule Matombo lakini "Location" kila akipost anachagua sehemu kali kali kuna maigizo mengi sana. Kuna Darasa la 7 mmoja kila siku anapost yuko "chuo cha Utalii" kumbe yuko Pugu Kajiungeni.

Ishi Maisha Yako, Yafurahie Maisha yako, Focus kwenye ndoto zako kuna siku watu watakuwa wanaku Post wewe bila kuwaomba waku Post... si unajua kibongo bongo Mtu anakufata Inbox anakuomba u Post Birthday yake anakutumia Picha na "Caption" ya wewe eti unamtakia Birthday njema na anaweza mind kichizi haujampost na Kumuwish.

Unaweza kutana na Mtu live akakuuliza "unanikumbuka" yule tumechat wote Insta leo, yaani Wale editor wa Picha Mungu anawaona mnawatengeneza watu wako soft kumbe uso live una makovu ya Tetekuwanga kichizi, kila Post anaandika "Njiro Uzunguni" kumbe tuko nae hapa mitaa ya Bibi Nyau Magomeni Makanya Karibu na Popo Bawa.

#Jikubali
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: