Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu, Bibi Winifrida Rutaindurwa akifungua mkutano wa wadau (hawapo pichani) wa kujadili marekebisho ya Sheria ya Tume ya Utumishi wa Walimu unaofanyika kwa siku mbili mjini Morogoro. Kulia ni Mkurugenzi wa Ajira na Maendeleo ya Watumishi, Bibi Christina Hape na kushoto ni Wakili Mkuu wa Serikali na Mkuu wa Kitengo cha Sheria, Tume ya Utumishi wa Walimu, Bw. Donald Chidowu
 Mkurugenzi wa Ajira na Maendeleo ya Watumishi, Tume ya Utumishi wa Walimu, Bibi Christina Hape akitoa ufafanuzi wa utendaji kazi wa Tume ya Utumishi wa walimu. Katikati ni Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu, Bibi Winifrida Rutaindurwa na kushoto ni Wakili Mkuu wa Serikali na Mkuu wa Kitengo cha Sheria, Tume ya Utumishi wa Walimu, Bw. Donald Chidowu.
 Wakili Mkuu wa Serikali na Mkuu wa Kitengo cha Sheria, Tume ya Utumishi wa Walimu, Bw. Donald Chidowu akiongea na wajumbe (hawapo pichani) katika mkutano wa kujadili marekebisho ya Sheria ya Tume ya Utumishi wa Walimu. Katikati ni Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu, Bibi Winifrida Rutaindurwa akifuatiwa na Mkurugenzi wa Ajira na Maendeleo ya Watumishi, Bibi Christina Hape.
 Washiriki wa Mkutano wa kujadili marekebisho ya Sheria ya Tume ya Utumishi wa Walimu wakisikiliza kwa makini maelezo ya Wakili Mkuu wa Serikali, Bw. Donald Chidowu (hayupo pichani) akifanua Sheria ya Tume ya Utumishi wa Walimu.
 Washiriki wa Mkutano wa kujadili marekebisho ya Sheria ya Tume ya Utumishi wa Walimu wakichukua dondoo muhimu wakati wa mkutano.
Afisa Sheria wa Tume ya Utumishi wa Walimu, Bw. Deogratias Haule akitoa maelezo katika mkutano wa kujadili marekebisho ya Sheria ya Tume ya Utumishi wa Walimu unaofanyika mjini Morogoro.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: