Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (MB) akizungumza na washiriki na watembeleaji wa maonesho ya Nanenane kanda ya Kaskazini.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (MB) akimshika ng’ombe aina ya Sahiwal alipotembelea banda la maonesho ya wanyama la Halmashauri ya wilaya ya Longido. (Kulia) Mkuu wa Mkoa wa Bw. Mrisho Gambo.
 Mjasiriamali Bi. Lilian Mhando akimweleza jambo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (MB) kuhusu unga wa mbegu za maboga alipotembelea banda la wajasiriamali waliopo SIDO. (Kushoto) Mkuu wa Mkoa wa Bw. Mrisho Gambo.
 Mjasiriamali Bi. Lilian Mhando akimweleza jambo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (MB) kuhusu unga wa mbegu za maboga alipotembelea banda la wajasiriamali waliopo SIDO. (Kushoto) Mkuu wa Mkoa wa Bw. Mrisho Gambo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (MB) akitoa zawadi kwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Bw. Jerry Muro (kushoto) baada ya Wilaya ya Arumeru kuwa mshindi wa pili kwenye uzalishaji wa mazao kanda ya kaskazini. (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU).

NA MWANDISHI WETU:

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (MB) amezitaka halmashauri kutambua mahitaji ya sekta ya kilimo, ufugaji na uvuvi ili kuleta mabadiliko chanya na maendeleo kwa sekta hizo nchini.

Hayo yamesemwa na Waziri huyo wakati akifunga maonesho ya wakulima na sherehe za nanenane kanda ya kaskazini Mkoani Arusha. Maonesho hayo yanafanyika katika uwanja wa Themi Njiro yakiwa na Kauli Mbiu: Wekeza katika Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa Maendeleo ya Viwanda.

Alieleza kuwa, Serikali ya awamu ya tano imeendelea kuonesha adhima ya dhati katika kuhakikisha wakulima, wafugaji na wavuvi wananufaika nchini. Serikali imeweza kufuta na kupunguza tozo na ada ambazo zilikuwa ni kero katika sekta hizo.

“Nimefurahi kuona bidhaa zinazozalishwa nchini katika sekta ya kilimo, ufugaji na uvuvi zinaubora wa hali ya juu, na hii inaashiria dhana ya viwanda vinavyozalisha nchini vinatumia teknolojia ya kisasa” alisema Mhagama

Aidha alitoa wito juu ya utunzaji wa mazingira, utatuzi wa migogoro ya wakulima, wafugaji na wavuvi, pamoja na viongozi na watendaji kushirikiana katika kutambua makundi ya vijana wenye viwango mbalimbali vya ujuzi na elimu, ili waweze kujifunza kupitia maonesho hayo, vilevile watengenezewe mfumo wa kuwabadilisha fikra kwenye suala la ajira kwa kutumia teknolojia zilizojidhihirisha kwenye maonesho hayo ili waweze kujiajiri na kutoa ajira kwa wengine.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Arusha alisema kuwa maonesho haya yamekuwa na manufaa kwa kuwahamasisha wakulima, wafungaji na wavuvi kuongeza uzalishaji na upatikanaji wa malighafi kwa ajili ya viwanda vilivyoanzishwa hapa nchini.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: