Mkurungenzi Mtendaji wa Sekta Binafsi nchini (TPSF), Godfrey Simbeye akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu Mkutano Mkuu wa Sekta hiyo utakaofanyika jijini Dar es Salaam August 28 wenye lengo lakujadili masuala ya Maadili na wimbi la Rushwa linaloikabili Sekta hiyo.

Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Majaliwa Kassim atarajia kukutana na Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF) na Wadau wake kujadiliana Maadali pamoja na masuala ya Rushwa ndani ya Sekta hiyo.

Katika Mkutano wake Mkuu wa Mwaka utakaofanyika August 28, 2018 jijini Dar es Salaam TPSF itajadili pia Changamoto zinazowakumba katika kufanya Biashara nchini.

Mjadala huo wa Maadili na Sakata la Rushwa utakaofunguliwa na Waziri Mkuu unafanyika ikiwa ni baada ya Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kufanya mazungumzo na Wafanyabiashara Desemba 3, 2015 na kugusia suala hilo kwa Wafanyabiashara hao.

Akizungumza na Waandishi wa Habari mapema leo, Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye amesema kuwa wanakutana kama Sekta Binafsi kujadili suala hilo, kutokana na kuwepo kwa tuhuma za vitendo ambavyo havina maadili katika Sekta hiyo mchini.

Simbeye amesema kusipokuwa na ushirikiano na kuaminiana kati ya Sekta ya Umma na TPSF hakutakuwa na maendeleo ya haraka.

Katika hatua nyingine, Simbeye ameahidi Sekta hiyo kusimamia ipasavyo Kanuni za maadili sambamba nakuacha kufanya vitendo vya rushwa vinavyotuhumiwa katika Sekta hiyo.

Pia Mkitano huo wa Wanachama wa Sekta Binafsi utatumia nafasi hiyo kumtafuta Mwenyekiti mpya wa TPSF baada ya Mwenyekiti wake aliyehudumu kwa kipindi cha miaka minne, Dkt Reginald Mengi kumaliza muda wake.

Kabla ya Mkutano huo, August 27, 2018 Kongano 14 zilizo katika Sekta hiyo zitapiga kura kumchagua Mjumbe mmoja atakayeingia kwenye Bodi ya TPSF ili kuwakilisha mawazo katika maendeleo ya Sekta Binafsi.

Bodi hiyo itazinduliwa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage ambapo watu 14 wanaowakilisha Kongano hizo atachaguliwa mmoja atakayekuwa Mwenyekiti wa TPSF.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: