WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Watoto na Wazee Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) kulia akimkabidhi madawati 40 Diwani wa Kata ya Chumbageni (CC) Saida Gadafi kwa ajili ya shule ya Sekondari Chumbageni ili kuweza kukabiliana na upungufu uliopo kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari Chumbageni Gabriel Habash.
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Watoto na Wazee Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) kulia akiwa amekaa kwenye mmoja ya madawati 40 aliyoyakabidhi leo kwa shule ya Sekondari Chumbageni kushoto ni Diwani wa Kata ya Chumbageni (CC) Saida Gadafi ambaye alimuomba Waziri huyo madawati hayoi kwa ajili ya shule ya Sekondari Chumbageni ili kuweza kukabiliana na upungufu uliopo.
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Watoto na Wazee Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) kushoto akifurahia jambo na wanafunzi wa shule ya Sekondari Chumbageni mara baada ya kuwakabidhi madawati hayo.
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Watoto na Wazee Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) akizungumza wakati wa halfa hiyo kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari Chumbageni Gabriel Habash na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Tanga
Thobias Mwilapwa.
Diwani wa Kata ya Chumbageni (CC) Saida Gadafi akizungumza katika halfa hiyo ambapo alimshukuru Waziri Ummy kwa kuwapa msaada huo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Sekondari Chumbageni Gabriel Habash akizungumza katika halfa hiyo ambapo alimshukuru Waziri Ummy kwa kuisaidia shule hiyo.
Mwalimu Mkuu wa wa shule ya Sekondari Chumbageni Kavumo Juma Mziray akitoa hotuba yake.
Sehemu ya wanafunzi wa shule hiyo wakifutiliana makabidhiano hayo.
Sehemu ya madawati na viti ambayo yamekabidhiwa leo na Waziri Ummy kwa shule ya Sekondari Chumbageni.
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Watoto na Wazee Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na waalimu wa shule ya Sekondari Chumbageni mara baada ya kukabidhi madawati hayo leo

NA MWANDISHI WETU, TANGA.

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Watoto na Wazee Ummy Mwalimu na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) leo amekabidhia madawati 40 na viti katika shule ya sekondari ya Chumbageni Jijini Tanga ikiwa ni mpango wake wa kuhakikisha changamoto zilizopo kwenye sekta ya elimu zinapatiwa ufumbuzi.

Halfa hiyo ya makabidhiano ilifanyika leo

shuleni hapo na kuhudhuriwa na walimu, wanafunzi na viongozi mbalimbali

akiwemo Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa ,Diwani wa Kata ya

Chumbageni Saida Gadafi wakiwemo viongozi wengine.
Hatua ya

kukabidhiwa madawati hayo shule ya Sekondari ya Chumnageni ilitokana na

ombi la Diwani wa Kata ya Chumbageni Saida Gadafi ambaye alimueleza

waziri Ummy uwepo wa uhaba wa madawati kwenye shule hiyo.
Akizungumza

namna alivyoweza kuipatia ufumbuzi changamoto hiyo, Waziri Ummy alisema

baada ya ombi hilo aliwapata wadau wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya

Jamii (NSSF) ambao walilikubali na kumpatia kiasi cha sh, milioni 5.4

ambazo wameweza kununua madawati 40 na viti
“Mh Saida umetenda

wajibu wako ipasavyo maana taarifa ya mkuu wa shule inasema kuna uhaba

wa viti 163ubawa wa meza 100 hivyo kupatina kwa hivyo vilivyokabidhiwa

leo kumepunguza nusu lakini nitaendelea kushirikiana nanyi “Alisema“Kazi

nzuri inafanywa kwenye shule ya sekondari Chumbageni na nimeambiwa

kiwango cha ufaulu kinaongezeka mwaka hadi mwaka asilimia 51 hadi

asilimia 77 lakini pia nitoe pongeze kwa Halmashauri ya Jiji la Tanga

kutatua changamoto ya elimu sio watu kusubiri mpaka serikali kuu kwani

wamekuwa wakijiongeza na diwani Saida kutatua changamoto ya elimu kwenye

kata yake “Alisema.
Hata hivyo alisema ataendelea kushirikiana

na madiwani kuhangaika ili aweze kupata fedha za ujenzi wa ofisi ya

walimu kwen ye shule hiyo lakini pia wanafunzi nitawaletea vitabu huku

akitoa wito kwa wananchi kushirikiana kuona namna ya kutatua changamoto

ya elimu sio kusubiri serikali pekee bali ni watu wote.
“Nimshukuru

Rais kuanzisha sera ya elimu bure ambayo imewasaidia, watu wengi

...watu walikuwa wanaponda shule za kata wakati mimi nilipokuwa nasoma

shule zikuwa chache kutokana na kukosekana nafasi lakini leo hii zipo za

kutosha hivyo kuwasaidia watoto wa kike kuepushwa na ndoa za utotoni na

wavulana kuvuta bangi.
Alisema leo hii Serikali chini ya Rais

Dkt John Magufuli imekuwa ilileta milioni 161 kila mwezi kwa Halmashauri

ya Jiji la Tanga kwa ajili ya elimu bure hii imesaidia sana lakini

wengine walikuwa wanakosa kwa sababu ya ada lakini tatizo la ada

limetatuliwa .
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: