Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina kushoto akipokea zawadi ya mtungi wa kiasili kutoka kwa Balozi wa Japan nchini, Masaharu Yoshida mara baada ya kufanya mazungumzo katika ofisi ndogo ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi jijini Dar es Salaam leo. Picha na Mpiga Picha Wetu.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akisisitiza jambo wakati akizungumza na watendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) kuhusu mchango wa sekta binafsi katika maendeleo ya sekta za mifugo na uvuvi alipowatembelea ofisini kwao Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi
wa TPSF, Godfey Sembeye. Picha na Mpiga Picha WetuWaziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Florens Luoga (kushoto) na Naibu Gavana wa Benki Kuu anayeshughulikia Uchumi na Fedha, Dk. Yamungu Kayandabila mara baada ya kufanya mazungumzo na watendaji wa benki hiyo alipowatembelea ofisini kwao Dar es Salaam.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina (kulia) akifurahia jambo na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Florens Luoga (kushoto) mara baada ya mazungumzo yaliyofanyika makao makuu ya BOT Dar es Salaam . 
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina (kulia) akiagana na Balozi wa Japan nchini, Masaharu Yoshida mara baada ya kufanya mazungumzo katika Ofisi ndogo za Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dar es Salaam
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: