Zoezi la ukaguzi wa majengo yanayojengwa katika kituo cha afya Mwela
Wanafunzi wa shule ya sekondari Tongani wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo alipotembelea shuleni hapo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo akiwa na viongozi na watendaji wa wilaya ya Pangani katika ukaguzi wa miradi ya maendeleo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo ameagiza kuondolewa kwa Mkandarasi anayejenga Ofisi za halmashauri ya wilaya ya Pangani kutokana na kushindwa kukamilisha Ujenzi huo kama mkataba unavyoelekeza. Waziri Jafo ametoa maelekezo hayo kwa viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Pangani wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya leo wilayani humo.

Mkandarasi huyo alianza kazi hiyo Novemba 2017 na alipaswa kukamilisha kazi hiyo juni 2018 lakini alishindwa kukamilisha na halmashauri kumuongezea muda hadi Agosti 31, mwaka huu. Licha ya kuongezwa Waziri Jafo amekuta hakuna chochote cha maana kilichofanyika na hivyo kuagiza kuondolewa kwa Mkandarasi huyo ili kumpata mtu makini wa kukamilisha kazi hiyo.

Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu amethibitisha kwamba Mkandarasi huyo hana uwezo kwa kuwa mara kadhaa amekuwa akikagua mradi huo na kutoa maelekezo lakini Mkandarasi huyo ameshindwa kutimiza wajibu wake.

Katika ziara hiyo, Waziri Jafo ametembelea miradi mingine na na kukasirishwa na utekelezaji ubovu wa mradi wa Ujenzi wa madarasa na mabweni kwa shule ya sekondari Tongani ambao ulipatiwa Sh.Milioni 259 mwaka jana na serikali lakini mradi huo hadi sasa haujakamilika. Kufuatia hali hiyo,

Waziri Jafo ameagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuchunguza wote waliohusika na kuwafikisha katika vyombo vya Dola. Hata hivyo Jafo amempongeza Mkuu wa wilaya hiyo kwa kuanza kuchukua hatua za uchunguzi juu ya watu waliohujumu mradi huo. Aidha, waziri Jafo amewataka wananchi wa wilaya hiyo kumuunga mkono Mbunge wao Jumaa Aweso kwa kuwa amekuwa akipigania upatikanaji wa miradi ya maendeleo kwenye jimbo hilo.

Kadhalika, amewataka wananchi wa Mwela pamoja na Mkaramo kushikamana na serikali ili kukamilisha ujezi wa vituo vya afya vilivyopata sh. milioni 400 kila kimoja kutoka serikali kuu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: