Wanataaluma MUHAS na wanajumuia wengine wa Muhimbili wakiandamana kusindikiza mwili wa marehemu Prof. Emil Namakuka Kikwilu kuelekea graduation square, MUHAS kwa ajili ya tukio la kumuaga.
 Wanataaluma wa MUHAS wakibeba mwili wa marehemu Prof. Emil Kikwilu kuelekea kwenye eneo malaamu kwa ajili ya tukio la kumuaga.
 Viongozi MUHAS na MNH wakifuatilia sala iliyoongozwa na wanafunzi wa Jumuia ya Katoliki Muhimbili, kabla ya kuaga mwili wa marehemu Prof. Emil Kikwilu.
 Ndugu wa marehemu Prof. Emil Kikwilu
 Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. Andrea Pembe akitoa salamu za Chuo
 Viongozi, Wanataaluma na wafanyakazi wengine wakiaga mwili wa marehemu Prof. Emil Kikwilu katika eneo la Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi, MUHAS
 Mke wa marehemu Prof. Kikwilu akipita kutoa heshima ya mwisho
 Waombolezaji mbalimbali wakifuatilia tukio la kumuaga Prof. Emil Kikwilu katika eneo la Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi, Muhimbili
Mkuu wa Skuli ya Afya ya Kinywa na Meno, Dkt. Elison Simon akimkabidhi mke wa marehemu Prof. Emil Kikwilu rambirambi kutoka kwa wafanyakazi wa MUHAS.

Chuo Kikuu cha afya na Sayansi Shirikishi Muhmbili (MUHAS) pamoja na jumuia yote ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) leo wameaga mwili wa marehemu Prof. Emil Namakuka Kikwilu, katika eneo la graduation square, MUHAS.

Tukio hili la kuaga mwili wa marehemu Prof. Kikwilu lilitanguliwa na maandamano ya wanataaluma ili kumuenzi mwanataaluma mwenzao kwa mchango wake katika taaluma.

Pamoja na kutoa salamu za pole kwa familia ya marehemu kwa kuondokewa na mpendwa wao, Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. Andrea Pembe alisema marehemu Prof. Emil Kikwilu atakumbukwa kwa utayari wake wa kufanya kazi kwa uhodari mkubwa wakati wote alipohitajiwa hasa katika kamati nyingi ambazo aliwahi kuteuliwa na Chuo, na siku zote alitoa mchango wenye hekima na uliosaidia kufanya maamuzi endelevu kwa Chuo. 

"Sisi kama Chuo tumepokea taarifa za kifo hiki kwa masikitiko makubwa hasa ukizingatia jinsi ambavyo mchango na busara zake bado tulikuwa tunazihitaji sana kwa ustawi wa Chuo chetu, na hasa katika Hospitali yetu mpya ya Taaluma na Tiba katika Kampasi ya Mloganzila" aliongeza Prof. Pembe.

Akizungumza katika tukio hilo, Mkuu wa Skuli ya Afya ya Kinywa na Meno, Dkt. Elison Simon alimuelezea marehemu kama mtu mchapa kazi na aliyetoa muda wake mwingi kusaidia watu wote bila kubagua. Dkt. Simon alisema kutokana na juhudi zake za kujituma na kujitolea, Prof. kikwilu alitambulika ndani na nje ya nchi na hivyo kupatiwa tuzo na shirika la kimataifa la Miracle Corners of the World liliko New York, Marekani.

Naye mwakilishi kutoka Chama cha Madaktari wa Afya na Kinywa na Meno Tanzania, TDA, alielezea masikitiko yao makubwa kwa kuondokewa na nguzo muhimu sana katika masuala ya afya ya kinywa na meno hapa nchini. 
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: