MHESHIMIWA Jaji Dkt. Eliezer M.Feleshi, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, (aliyesimama) akitoa hotuba ya ufunguzi wa mafunzo kwa mahakimu wakazi wa wilaya na mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara na Morogoro kuhusu Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi Sura 263 marejeo ya mwaka 2015 iliyoanza Septemba 5, 2018 mkoani Morogoro. Semina hiyo imeratibiwa kwa ushirikiano wa Chuo Cha Uongozi wa Mahakama Lushoto na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF). Wengine pichani ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, ambaye pia ni Mkuu wa Chuo hicho Dkt. Paul F. Kihwelo (kulia) na Mkurugezni Mkuu wa WCF, Bw.Masha Mshomba.
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, akizungumza kwenye semina hiyo.
Baadhi ya Wahwshimiwa Mahakimu Wakazi Wafawidhi wa Mahakama nchini.
Mheshimiwa Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Kisarawe Mkoani Pwani, Mhe. Devota Kisoka.
Mhe. Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mtwara, Bi.Elizabeth S. Missana, akipitia kipperushi chenye maelezo kuhusu shughuli za Mfuko.
Baadhi ya Waheshimiwa Mahakimu Wakazi Wafawidhi wa Mahakama nchini.
Hakimu Mfawidhi wa Mahaka ya Hakimu Mkazi Morogoro, Mheshimiwa Elizabeth Nyembele, akizungumza kwenye semina hiyo.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Kibaha, Mhe.Joyce J. Mkhoi, akitoa maoni yake kwenye semina hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, akishauriana jambo na Mkuu wa Huudma za Sheria wa Mfuko huo, Bw.Abraham Siyovelwa.
Bw. Mshomba (katikati), akimtambulisha Dkt. Feleshi kwa Mkurugenzi wa Uendeshaji WCF, Bw. Anselim Peter, wakati akiwasili ukumbini.
Dkt. Feleshi akisalimiana na Bw. Siyovelwa.
MHESHIMIWA Jaji Dkt. Eliezer M.Feleshi, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, (kushoto), na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Masha Mshomba, wakiwa na furaha baada ya Dkt. Felishi kufungua mafunzo ya kujenga uwezo na uelewa wa sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi Kifungu namba 5 [Sura ya 263 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2015] kwa mahakimu Wakuu Wakazi wa Mikoa na Wilaya kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Lindi na Mtwara. Semina hiyo iiyoandaliwa kwa ushirikiano kati ya Chuo Cha Uongozxi wa Mahakama Lushoto na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) imeanza Septemba 5, 2015 mjini Morogoro.
Kutoka kushoto ni Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Mhe. Godfrey Isaya, Mhe. Dkt. Feleshi, Mhe. Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, Mhe. Dkt. Jaji Paul Kihwelo, Mkuu wa Huduma za Sheria WCF, Bw. Abraham Siyovelwa.
Mkuu wa Huduma za Sheria WCF, Bw. Abraham Siyovelwa, akitoa mada kuhusu sharia zinazosimamia Mfuko huo.
Mkurugenzi wa Uendeshaji WCF, Bw. Anselim Peter, akitoa mada.
Afisa Uhusiano na Mawasiliano Mwandamizi wa WCF, Bw. Sebera Fulgence, akiongoza semina hiyo.
MHESHIMIWA Jaji Dkt. Eliezer M.Feleshi, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, akisalimiana na Afisa Sheria wa WCF, Bw. Deo Victor.
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, ambaye pia ni Mkuu wa Chuo Dkt. Paul F. Kihwelo, (kulia), akisindikizwa na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro, Mhe.Elizabeth Nyembele, (kushoto) na Afisa Sheria wa WCF, Bw. Deo Victor.
Mhadhiri Msaidizi wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA), Mhe.Lamek Samson akiwa na Afisa Uhusiano na Mawasiliano Mwandamizi wa WCF, Bw. Sebera Fulgence.

Na K-VIS BLOG/Khalfan Said, Morogoro.

MHESHIMIWA Jaji Dkt. Eliezer M.Feleshi, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, amesema hategemei kesi zinazohusiana na masuala ya fidia kwa wafanyakazi zikichelewa pindi mashauri yake yanapofika mahakamani.

Dkt. Feleshi ameyasema hayo Mjini Morogoro Septemba 5, 2018 wakati akifungua mafunzo kwa mahakimu kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Mtwara, Lindi na Morogoro yanayoratibiwa na Chuo Cha Uongozi wa Mahakama Lushoto na kuendeshwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) yanayofanyika kwa siku mbili kuanzia leo.

“Sitegemei kesi za namna hii ziingie kwenye kundi la njoo kesho… njoo kesho, mashahidi wake ni wangapi? Kesi za namna hii zikiingia zisikilizwe mfululizo, kumbukeni inamuhusu mtu aliyeumia, inagusu uhai, inahusu
ulemavu wa kudumu kwa hiyo nyuma kuna wategemezi na yeye mwenyewe kwa hiyo inahusu maisha ya mtu, pia ushahidi wake uko wazi na adhabu zake ziko bayana” Alifafanua Dkt. Feleshi.

Aidha Mhe. Jaji Kiongozi alisema, kila mfanyakazi aliyeumia au kuugua kutokana na kazi anayo haki ya kupata fidia stahiki na kwa wakati kwa mujibu wa sheria na kwa yule atakayefariki katika mazingira hayo basi wategemezi wake nao wanapatiwa haki zao zilizoanishwa kisheria.


Alisema huduma ya Hifadhi ya Jamii ni haki inayotambulika na kulindwa na Katiba, ibara ya 11 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 pamoja na mambo mengine inatamka kwenye ibara ndogo kwamba Mamlaka ya Nchi itaweka utaratibu unaofaa kwa ajili ya kufanikisha utekelezaji wa haki ya mtu kufanya kazi, haki ya kujipatia elimu na haki ya kupata msaada kutoka kwa jamii wakati wa uzee, maradhi, au hali ya ulemavu na katika hali nyinginezo za mtu kuwa hajiwezi, na bila kuathiri haki hizo Mamlaka ya Nchi itaweka utaratibu wa kuhakikisha kwamba kila mtu anaishi kwa jasho lake.

“Hayo ni maneno ambayo yamewekwa kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa hiyo ni haki ambayo imetamkwa na inalidwa na Sheria na kwa kuzingatia matakwa hayo ya kikatiba ndio maana ilitungwa sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi iliyoanzisha Mfuko huu wa WCF.” Alifafanua Dkt. Feleshi.

Alisema Mafunzo hayo kwa Mahakimu kuhusu utekelezaji wa sheria hiyo, yana manufaa makubwa na ndio maana yameratibiwa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama ambacho ndio chenye jukumu la kutoa elimu kwa watumishi wa mahakama.

“Katika sheria ya sasa kwa mujibu wa vifungu vya 22 (1) 46 na 48 na majedwali ya 2,3 na 4 ulipaji wa fidia unazingatia zaidi uhalisia wa tukio, kiwango cha hasara na
madhara ambavyo vinafanya fidia inayolipwa ikokotolewe kwa kufuata asilimia ya vigezo hivyo na malipo ya ujira wa mwezi au malipo ya mwisho ya mhusika.” Alibainisha Dkt. Feleshi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: