Shule ya Sekondari ya wasichana ya John Baptist imefanya mahafali ya kidato cha nne na kushuhudia jumla ya wanafunzi 32 wakihitimu kidato cha nne. Shule hiyo pia ilitumia mahafali hayo kuzindua rasmi masomo ya kidato cha tano na sita kwa wasichana.
Akizungumza kwenye mahafali hayo mgeni rasmi ambaye ni Rais wa Chemba ya Biashara Tanzania Octa Mshiu alisema " wasichana ni nguzo kuu ya maendeleo ya Taifa letu, tunawaomba muende kutumia maarifa mliyoyapata hapa na muhimu zaidi ni kuendelea kukumbuka kuwa hakuna litakalowezekana bila ya kutilia maanani nidhamu na kufanya kazi kwa bidii.
Naye Mkurugenzi wa shule hiyo Jalia Mayanja alisema shule ya John Baptist imenuia kusaidia wasichana kufikia malengo yao kutumia elimu na kutilia mkazo nidhamu. Aliwakaribisha wazazi kutumia shule hiyo kwa ajili ya masomo ya watoto wao kwa kidato cha tano na sita yaliyoanzishwa. Shule hiyo inayotoa michepuo ya ECA, HKL na HGE na iko Boko Jijini Dar es Salaam.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: