Na Ripota Wetu, Globu ya jamii

MAKONTENA ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ambayo yamebeba samani za walimu yameanza kupigwa mnada.

Hatua ya kupiga mnada makontena hayo inakuja baada ya Rais Dk.John Magufuli kutoa maagizo ya kuhakikisha yanalipiwa kodi na ikishindikana yapigwe mnada.

Rais Dkt. Magufuli alitoa kauli hiyo juzi akiwa mkoani Chato na sababu za kutoa ufafanuzi na maelekezo hayo baada ya kuona Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam analazimisha makontena hayo yatolewe bila kulipiwa kodi.

Hivyo leo makontena hayo yameanza kupigwa mnada kuanzia saa tatu ya asubuhi na unafanyika bandari ya Dar es Salaam upande wa Malawi Cargo.

Mnada huo tangu ulipoanza asubuhi unaendelea kufanyika hadi sasa.

Katika mnada huo wananchi, taasisi,mashirika na baadhi ya viongozi wa Serikali wamejitokeza kwa lengo la nununua samani zilizopo kwenye makontena hayo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: