Mwanamuziki mashuhuri wa reggae nchini Uganda, Moses Sali, maarufu kwa jina la steji 'Bebe Cool' amejikuta katika wakati mgumu wa kurushiwa machupa ya maji ili ashuke stejini baada ya kauli yake ya kumbeza mwanasiasa Bobi Wine.

Sakata hilo limetokea wikendi iliyopita katika tamasha moja lililofanyika nchini humo, ambapo msanii huyo amesema kuwa "Mbunge BobiWine kuwa anajionesha kuwa amejeruhiwa sana ili kupata huruma za wananchi na jumuiya ya kimataifa,"

Kufuatia kauli hiyo, mashabiki walimzomea na kuanza kumrushia machupa ya maji na kupelekea msanii huyo kusitisha kitumbuiza. Bebe Cool ni rafiki wa karibu wa Rais Museveni.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: