Gari la lilokuwa limebeba waandishi.
Msafara wa Rais Dkt. John Magufuli uliokuwa ukielekea wilayani Ukerewe mkoani Mwanza, umepata ajali katika Kijiji cha Kasuguti, kata ya Kisorya, wilayani Bunda mkoani Mara, leo Septemba 4, 2018 baada ya magari manne kugongana katika eneo ambalo barabara ilikuwa ikijengwa.

Taarifa za awali zinadai kuwa, waandishi wawili wa habari wamejeruhiwa baada ya gari walimokuwa kupinduka.

Kwa mujibu wa Mkuu Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Mara, R.T.O Steven akizungumza na wanahabari kwa njia ya simu amethibitisha kutokea kwa ajli hiyo na kusema kuwa miongoni mwa gari zilizopata ajali moja ni waandishi wa habari na nyingine ni ya TAKUKURU.

Amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni vumbi lilikuwa limetapakaa barabarani kutokana na msafara huo hivyo madereva kushindwa kuona vizuri njia lakini hakuna madhara makubwa licha ya gari moja kubondeka ubavuni baada ya kupinduka.

Ameongeza kuwa, magari yote yameshafika eneo la ambalo Rais Dkt. Magufuli amekwenda kufanya ziara wala hakuna taarifa ya mtu aliyepelekwa hospitali kwa kuumia.

Taarifa nyingine kutoka eneo la tukio zinadai kwamba gari lingine lililopata ajali ni la Chama Cha Mapinduzi mkoa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: