Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) kupitia programs ya Dawati la Jinsia Wanawake na watoto yagawa vifaa vya Umeme wa JUA kwa watoto wa kike Wilaya ya Gairo.

Mratibu wa CCT Gairo Bw. Peter Kihiyo akiongozwa na Mkurugenzi wa Dawati la Jinsia mama Mbena walionesha jinsi CCT inavyoguswa na mateso ya mtoto wa kike hasa wale wanyonge.

CCT walikabidhi vifaa hivyo kwa wanafunzi katika tukio ambalo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Shaidi Mchembe.

CCT kupitia Dawati la Jinsia linafanya kazi kwa karibu kabisa na Wilaya ya Gairo katika kutokomeza mimba/ndoa za utotoni, ukeketaji, utoro na ubakaji.
Elimu zinatolewa kila kona na wananchi wa Gairo wamehamasika katika kumlinda mtoto wa kike.

Kati ya shule zilizopata vifaa hivyo ni Gairo Sec ambayo ina kidato cha tano na sita kwa mabinti.

Aidha CCT ilienda mpaka vijijini kiwatembelea wanafunzi wa kike waliobainishwa kutoka kwenye familia zenye umasikini wa kutupa. Lengo ni ili nao wajisomee nyakati za usiku kama wenzao ili kupata ushindani sawia.

Hii ni mikakati ya kumkomboa mtoto wa kike kuanzia kwenye MISINGI hatimaye tufikie 50 kwa 50 SDG namba 5. Misingi ikiharibika mwenye haki atafanya nini?

Mhe. Mchembe aliwapongeza sana CCT kwa kuwa sehemu ya wadau wakubwa wa maendeleo Gairo kupitia kilimo, utawala bora, IR-Vicoba na dawati la Jinsia.

Aidha wakiwa kama walezi wakuu wa Jukwaa la Amani Dini Mbalimbali wameendelea kuifanya Gairo chombo cha Amani katika Taifa.
Mhe. Mchembe aliomba salamu za wana Gairo zimfikie Katibu Mkuu CCT Canon Moses Matonya na uongozi wote. Wananchi wa Gairo wanawashukuru sana CCT kwa upendo na ukarimu wao mkubwa.

Aidha, aliwaasa watoto hao wa kike kuzingatia masomo na kujitambua kwani kesho yao ipo mikononi mwao wenyewe, “kupanga ni kuchagua”.

Vyombo hivyo vitunzwe na vitumike katika makusudi yanayotakiwa ili kuwaletea matokeo ChanyA+.

Watoto wa kike ni nguzo imara ya pambo katika kuta za nchi ya Tanzania. Watoto wa kike walindwe
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: