Prof Paramagamba Kabudi kaongea vitu ambavyo huwezi kusoma UDSM wala Mzumbe. Tuna watu wengi nguli kama Prof Kabudi kwa nyanja mbalimbali. Changamoto ni namna gani wanatupa fursa ya kunyonya wanayoyajua.

Pia rika lao ndio limezeeka. Ni fahari taifa kuwatumia na kuwaenzi hawa Wazee kwa waliopo hai , ili tuweze kunyonya kutoka kwao. Wapo wazee wengi wastaafu na hatuwatumii kusema la kweli.
Kupitia midahalo ndiyo njia pekee ya kuelimisha hiki kizazi kisichojua HISTORIA ya United Republic of Tanzania,Tanzania na Tanganyika.

Kabudi ni mtoto wa Tanzania. Uwezo wake umewakilisha uwezo wa Watanzania.

"Ipendeni nchi yenu, itakieni mema, isaidieni isonge mbele, Mliwadekeza wenzenu, mlipowekeza walidhani ni msaada, sasa mkiwekeza sasa simamieni miradi yenu, waongozeni ndugu zenu,hii ndio michango tunayoitarajia toka kwenu "

"Njooni na skills zenu msaidieni pale mnapoona bado hapanogi, kama mnataka matembele waambieni wayakaushe matembele wawaleteeni huku Ulaya "

"Hamna nchi nyingine msijidanganye ni Tanzania, Serikali ya awamu ya tano inawathamini sana, kuweni wazalendo isaidieni nchi yenu, ninyi ni ndugu zetu na sisi ndio ndugu zenu "

"Wakati unazungumza Mh Kabudi, Mh Rais kanitumia sms, wakati najibu kanipigia, kwa hakika ni Rais anayeipenda nchi yake kweli kweli, ameniambia yupo Chato anafuatilia mkutano wa diaspora toka jana, huu ni Ulimwengu wa kimtandao, wote waliozungumza amewasikia, anawapongeza wote na atatekeleza, tumpigie makofi Mh Rais."

"Ukizaa mtoto nje ya nchi hata kama wewe ni Mtanzani na mkeo Mtanzania, mtoto wenu atakuwa raia wa kurithi kutokana na wazazi wenu na atakosa haki ya kugombea Urais wa Tanzania."

"Ninyi mko huku Seattle, Marekani ila mimi nimeongoza mabaraza ya sheria na katiba maeneo yote ya mipakani na wenzetu wanaoishi mipakani walikataa kata kata uraia pacha kwa sababu ya Usalama wao "

"Nilikaa Ujerumani miaka 10 nilibakisha miaka kadhaa kuwa na haki ya kuishi Ujerumani muda wote lakini nikasema no, mke wangu kamaliza PhD twende turudi nyumbani, off course kwa sababu ya ubaguzi pia, Mwanangu anakuwa wa kwanza darasani wazungu hawaelewi kwa nini mwafrika anakuwa wa kwanza, sasa walitaka awe wa mwisho, mwingine kila siku ananifundisha kutumia photocopy mashine mwanzo nilikasirika ila nilipoona nimepata mfanyakazi wa kunisaidia kupiga Copy nikatulia tu, sasa najiuliza hivi walidhani mimi mkubwa mzima nashindwa kupiga copy "

"Huyu Mayor wa Seattle namheshimu, tumenunua ndege mbili tena Cash, pale airport waliniambia you are a government officer, nikamrekebisha Yule bwana nikamwambia not only a government officer, Am a Minister of respective country"

"Maendeleo yapimwe sio kwa kuangalia kimo bali shimo tulikotoka. Tanzania imetoka mbali."
Prof. Kabudi.

_Viva Tanzania vivaaaaaaaaaa _
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: