Miss Tanzania 2016 Diana Edward akikabidhi taji kwa mshindi wa Miss Tanzania 2018 Queen Elizabeth baada ya kutangazwa akiwabwaga walimbwende wengine 19.
Miss Tanzania 2016 Diana Edward akikabidhi taji kwa mshindi wa Miss Tanzania 2018 Queen Elizabeth baada ya kutangazwa akiwabwaga walimbwende wengine 19
Miss Tanzania 2018 Queen Elizabeth akiwa na washindi wa pili na wa tatu baada ya kuvalishwa rasmi taji la Miss Tanzania usiku wa jana kwenue Ukumbi wa Kimataifa wa Mwl Julius Nyerere Jijini Dar.
Majaji wa Miss Tanzania 2018 wakifuatilia kwa makini shindano hilo jana usiku.
Walimbwende wa Miss Tanzania 2018 wakipita jukwaani katika mashindano yaliyofanyika usiku wa Jana kwenye ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa wa Mwl Julius Kambarage Nyerere.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Kinyang'anyiro cha kumpata mrembo wa Miss Tanzania 2018 limefanyika jana usiku na Mrembo kutoka Kinondoni Queen Elizabeth amefanikiwa kuondoka na taji hilo katika shindano lililofanyika jana usiku kwenye Ukumbi mpya wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Saalaam.

Katika shindano hili, Mshindi wa pili ni Nelly Kazikazi na mshindi wa tatu ni Sandra Giovinazzo.

Baada ya kuibuka na ushind wa taji la Miss Tanzania 2018, Queen Elizabeth ameweka wazi mwanzo mwisho kile kilichopelekea kushinda taji hili la U-Miss kwa walikuwa wanashindana na warembo wengi halafu wazuri.

“Nafurahia kushinda taji hili la Miss Tanzania 2018, najisikia vizuri sana napenda kuwashukuru majaji kwa kuweza kuona nafaa kuiwakilisha nchi nasema asante Tanzania, ukiwa kama mrembo lazima ujiandae kama unavyoona warembo ni wazuri sio kwamba ni wazuri kumuonekano tu hata kichwani pia wako vizuri” Queen alisema.

Katika shinda no hilo Queen Elizabeth amewashinda warembo wengine 19 waliokuwa wakiliwinda taji hilo kubwa kabisa nchini katika tasnia ya urembo.

Shindano la Miss Tanzania 2018 liliweza kuhudhuriwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga, Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe akiwa moja ya zao la Miss Tanzania 2006 na kuibuka namba mbili Jokate Mwegelo pamoja mbunge wa Segerea Bona Kaluwa.

Waziri Mwakyembe amesema kuwa, mashindano ya mwaka huu yamekuwa na tija kubwa sana kutokana na waandaaji wa mwaka huu chini ya Basila Mwanukuzi kujipanga na kushirikiana na serikali kuanzia hatua ya mwanzo mpaka kufikia tamati.

Warembo watano waliofanikiwa kuingia tano bora wamepewa ubalozi wa mwaka mmoja na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) na Wakala wa Misitu Nchini (TFS).
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: