Na Mwandishi Wetu

Jumuiya ya wafanya biashara wanaoisho nchini China wasifu utendaji mzuri wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Akizungumza kwa niaba ya Jumuiya ya Wafanyabishara katika kikao cha Waziri Mkuu na watanzania wanaoishi nchini China Bw. John Ruhumbiza alisema wafanyabishara waishio nchini China wanaunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya Tano katika kuletea maendeleo ili kuifikisha Tanzania katika uchumi wa kati.

"Tunaunga mkono juhudi za Serikali katika kuleta maendeleo na kuiwezesha nchi kufikia uchumi wa kati".

Aidha alieleza kuwa utendaji wa Mhe. Rais umeiletea Tanzania heshima kubwa kwa kusaidia kuimarisha mahusiamo ya wafanya biashara waliopo China na Kampuni mbalimbali za China.

Vile vile amesema kuwa Tanzania ni soko kubwa la bidhaa zinazotoka China lakini kupitia umoja wa Wafanyabiashara waishio China wanapata fursa ya kujua ni bidhaa gani za Tanzania zinaweza kupata soko nchini China.

Hata hivyo aliiomba Serikali ya Tanzania kuzungumza na Serikali ya China kuendelea kuweka mazingira mazuri ya kibiashara kwa watanzania hasa katika masuala ya kupata leseni za biashara na vibali vingine.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: