Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Isaack Kamwelwe, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka, Mawaziri pamoja na viongozi wengine akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mitambo itakayotumika katika ujenzi wa barabara ya Bariadi-Maswa km 49.7 itakayojengwa kwa kiwango cha lami mara baada ya kuweka jiwe la msingi Bariadi mkoani Simiyu.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono mamia ya wananchi wa Bariadi waliohudhuria katika sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi katika ujenzi wa barabara ya Bariadi-Maswa km 49.7 itakayojengwa katika kiwango cha lami

Sehemu ya Wananchi wa Bariadi waliohudhuria katika sherehe hizo za uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa barabara ya Bariadi-Maswa km 49.7 itakayojengwa katika kiwango cha lami
 Katapila likiwa linaendelea na kazi ya ujenzi wa barabara ya Bariadi-Maswa km 49.7 itakayojengwa katika kiwango cha lami katika eneo la Bariadi mkoani Simiyu.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Bariadi katika sherehe hizo za uwekaji wa jiwe la msingi.
 Mbunge wa Bariadi Andrew Chenge akifurahia jambo na Mbunge mwenzake wa Misungwi Charles Kitwanga wakati wa hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika sherehe za uwekaji wa jiwe hilo la msingi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiondoka mara baada ya kuweka jiwe la msingi mradi wa barabara ya Bariadi-Maswa km 49.7, Bariadi mkoani Simiyu. PICHA NA IKULU.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: