Mradi wa Kuwawezesha vijana wa kike na wanawake kiuchumi kupitia Tasnia ya Urembo na Vipodozi ujulikanao kama Manjano Dream-Makers ulioasisiwa na Taasisi ya Manjano Foundation wamemaliza mafunzo ya ujasiriamali kwa wanawake wa Mkoa wa Kigoma Yaliofanyika kwa wiki mbili kwenye ukumbi wa SIDO Mkoani Kigoma. Mafunzo hayo yaliyotolewa bure yamewanufainsa wanawake 20 kutoka Mkoani Kigoma na vitongoji vya jirani.
Mafunzo hayo yalikuwa na lengo la kumsaidia mjasiriamali mwanamke kujikwamua na kujiongezea kipato. Awamu ya kwanza ni kumfundisha maswala ya biashara namna ya kuibua na kubuni miradi mbalimbali namna ya kuandika mpangilio wa biashara ikiwemo matumizi sahihi ya rasilimali muda, kutokufuja fedha na pia namna ya kujitunzia akiba itokanayo na biashara yake.

Awamu ya pili walipata ujuzi jinsi ya kupamba ma harusi na matumizi sahihi ya vipodozi salama vya LuvTouch Manjano.
Baada ya wanawake hawa kuhitimu mafunzo haya Taasisi ya Manjano Foundation itawaunganisha na taasisi za fedha zinazotoa mikopo bila riba ili waweze kupata mtaji wa kununua bidhaa za vipodozi kwa ajili ya kuwawezesha kuanzisha biashara zao wakiwa chini ya uangalizi maalum wa Taasisi hiyo kwa lengo la kuhakikisha kila mhitimu wa mafunzo haya anapiga hatua na kuweza kujitegemea.

Taasisi ya Manjano imefanikiwa kuwawezesha zaidi ya wanawake 500 kutoka Mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Dodoma, Mbeya, Mtwara, Kigoma na Unguja - Zanzibar
Wengi wa wahitimu wa mradi wa Manjano Dream-Makers wamefanikiwa kuanzisha biashara zao na kuwa mawakala wa bidhaa za LuvTouch Manjano. Kwa mwaka huu taasisi ya Manjano wanajipanga pIa kumalizia kwa kuwawezesha kiuchumi na kutengeneza ajira kwa vijana wa kike na wanawake wa Mkoa wa Tabora..
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: