Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Prof. Lawrence Museru (kushoto) akizungumza na mke wa aliyekuwa Balozi wa Marekani Dkt Deborah Stith.

Wataalam kutoka vyuo vikuu mbalimbali nchini Marekani pamoja na wataalam wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wakifuatilia kwa makini katika mkutano huo.

Baadhi ya wakurugenzi wa (MNH) wakisikiliza kwa makini katika mkutano huo Mkuu wa Idara ya Macho Dkt. Mtemi Baruani (kushoto) na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Shirikishi Dkt Praxeda Ogweyo (kulia).

Na Mwandishi Wetu.

Wataalam wa Afya kutoka Marekani leo wametembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na kufanya mazungumzo na uongozi wa hospitali hiyo lengo likiwa ni kushirikiana katika utoaji wa huduma za afya.

Ujio huo wa wataalam 9 umeongozwa na mke wa aliyekuwa Balozi wa Marekani, Dkt. Deborah Stith akiwa na wataalamu hao wakiwemo madaktari wa macho, mfumo wa mkojo na meno.

Akizungumza katika mapokezi hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Lawrence Museru amesema lengo la ugeni huo ni kuangalia jinsi ambavyo pande hizi mbili zinavyoweza kunufaika kwa kujenga mahusiano katika ufundishaji ,kuboresha huduma pamoja na utafiti.

“Ushirikiano ambao tunautafuta hasa ni katika nyanja ya ufundishaji ikiwa ni pamoja na kuwaongezea ujuzi madaktari wetu katika sehemu tulizokuwa tunafikiri kutoa huduma ambazo tulikuwa hatutoi awali” Amesema Prof. Museru.

Aidha Dkt. Deborah Stith amesema wako tayari kushirikiana kwa karibu na Muhimbili kwa kubadilishana wataalam kwa manufaa ya jamii.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: