Na Elizabeth Edward, Mwananchi.


 Rais wa Tanzania, John Magufuli amesema Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye hawafai kuendelea na nyadhifa zao kutokana na mambo waliyoyafanya.

“Nitaendelea kuwapenda lakini kwenye nafasi zenu hapana. Watanzania mmenichagua kusimamia haki na utendaji kazi ndani ya Serikali ili kila fedha ya Watanzania iktumike kwa mujibu wa sheria,” amesema Rais Magufuli.

Kiongozi mkuu huyo wa nchi ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Januari 23, 2020 katika hafla ya uzinduzi wa nyumba za Jeshi la Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam huku akisisitiza kuwa tume nyingi zimeundwa kuchunguza miradi ya hovyo inayosimamiwa na Wizara ya Mambo ya Ndani.

Magufuli amesema kutokana na sakata hilo katibu mkuu wa wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu ameandika barua ya kujiuzulu na amemkubalia.

“Watu wamekosa uadilifu, hivi karibuni kulikuwa na mkataba mmoja wa ajabu unaotengenezwa Wizara ya Mambo ya Ndani wenye thamani ya zaidi ya Sh1 trilioni. Mradi huo umesainiwa na kamishna jenerali wa Zimamoto.”

“Haujapangwa kwenye bajeti na haujapitishwa na Bunge. Wakati wa vikao na kampuni moja ya Romania, wahusika wote wa Tanzania waliokuwa wanakwenda katika majadiliano na kulipwa Dola 800 za posho ya vikao,” amesema Magufuli, na kubainisha kuwa hata tiketi za ndege walilipiwa.

Amesema mkataba huo ni wa hovyo kwa sababu ili kuuvunja yaliyoanza kutekelezwa lazima yaendelee kutekelezwa.

“Lugola nampenda sana ni mwanafunzi wangu nimemfundisha Sengerema Sekondari pamoja na mwili na ukubwa wake lakini katika hili hapana. Nilitegemea hata hapa sitamkuta, nasema kwa dhati.”

“Andengenye nampenda sana, ni mchapakazi lakini kwenye hili hapana, nilitegemea asiwepo hapa. Hatuwezi kuendesha nchi kwa misingi ya ajabu namna hii. Yanayokwenda kununuliwa katika mkataba ni ya hovyo.”

Ameongeza, “nampongeza Kingu kwa kuwajibika na hii imempa heshima kwamba angalau ametambua, inawezekana haya hakuyafanya yeye lakini kwa kuwa yeye ni katibu mkuu amewajibika kwa hilo, nampongeza na nitaendelea kumheshimu.”

Magufuli ameshangazwa mtu kusaini Sh1 trilioni wakati jukumu la kukopa fedha ni la Wizara ya Fedha.

Amesema haiwezekani watendaji kufanya mambo wanavyotaka kwa kuwa wataipeleka nchi kubaya na kukiuka misingi na ilani ya uchaguzi ya CCM.

“Huo ndio ukweli na siku zote nitasimamia ukweli, Ndugu zangu ninajua hili…, wapo pia ofisi ya mwanasheria mkuu, walisubiri mwanasheria mkuu alipofiwa na mke wake wakaenda wakapitisha na kuandika kwa niaba na kwa niaba, wapo nao wanahusika.”


“Wapo wanaohusika katika wizara ya Mambo ya Ndani lakini kitendo cha Zimamoto na ni wasaidizi wa Andengenye ni lazima wajitathmini,” amesema Magufuli
Meneja wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kituo cha Tabora Bw. Daniel Nyimbo akielezea jambo kwa wanafunzi wa shule za sekondari za Tabora Boys na Tabora Girls walioshiriki warsha ya kuwajengea uwezo wanafunzi wa sekondari kuhusu sekta ya usafiri wa anga, hususani fursa za ajira zilizoko kwenye sekta hiyo. Zaidi ya wanafunzi 600 kutoka shule ya sekondari Mirambo, Tabora Boys na Tabora Girls wameshiriki Warsha hiyo.
Sehemu ya wanafunzi wa shule za sekondari za Tabora Boys na Tabora Girls walioshiriki warsha hiyo wakisikiliza maelekezo kutoka kwa wataalamu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania.
Mkufunzi Mkuu Kitengo cha huduma za viwanja vya ndege kutoka Chuo cha Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(CATC) kilichopo Dar es Salaam Bi.Thamarat Abeid akitoa ufafanuzi wa fursa za kimasomo katika chuo hicho pamoja na sifa za ujumla zinazohitajika ili kujiunga na masomo ya usafiri wa Anga kwa wanafunzi wa shule za sekondari za Tabora Boys na Tabora Girls walioshiriki warsha hiyo.
Picha ya pamoja baada ya warsha.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Milambo wakijiandaa kushiriki warsha ya kuwajengea uwezo wanafunzi wa sekondari kuhusu sekta ya usafiri wa anga, hususani fursa za ajira zilizoko kwenye sekta hiyo.
Picha ya pamoja baada ya warsha.
Mmoja wa wanawake waliojifungua katika hospitali ya Mwananyamala, Rebecca Nelson akifurahia Diapers mpya za Smiley baada ya kukabidhiwa na balozi wa bidhaa hizo za T-MARC Tanzania, Dinah Marrios (kushoto), wengine pichani ni watumishi waandamizi wa hospitali hiyo na kutoka taasisi yak T-MARC.
Mkurugenzi wa bidhaa za kijamii wa T-MARC Tanzania , Flavian Ngole, (kulia) akikabidhi msaada wa diapers mpya za Smiley zilizozinduliwa katika soko nchini karibuni na T-MARC, kwa mzazi, Rebecca Nelson, katika wodi ya wazazi ya hospitali ya Mwananyamala jijiji Dar es Salaam, wakati wa hafla ya taasisi hiyo kukabidhi msaada wa bidhaa hizo hospitalini hapo , (katikati) ni Balozi wa Smiley,   Dinah Marrios, wengine (kutoka kushoto) ni Muuguzi Mkuu wa Hospitali hiyo , Dk.Mussa Wambura na Muuguzi Rosa Moses.
Wauguzi Waandamizi wa hospitali ya Mwananyamala wakipokea msaada wa Diapers za Smiley zlizozinduliwa hivi karibuni kutoka kwa Mkurugenzi wa bidhaa za kijamii wa T-MARC Tanzania, Flavian Ngole (kushoto) na balozi wa bidhaa hizo, Dinah Marrios.
Maendeleo ya Ujenzi wa Barabara za Juu katika Makutano ya Ubungo (Ubungo Interchange). Mradi huo wa Ujenzi katika Makutano ya Barabara za Mandela, Morogoro na Sam Nujoma (Ubungo Interchange) unaendelea kwa kasi kubwa na umefikia asilimia 65 kwa mradi mzima na sehemu ya gorofa ya pili ambayo itapitisha magari yanayotumia barabara ya Morogoro imefikia asilimia 75. Mradi huo unatarajiwa kuondoa adha ya msongamano mkubwa katika makutano ya barabara hizo pindi utakapokamilika. 
Ujenzi wa reli ya kisasa SGR
Upanuzi wa Barabara ya Morogoro kwa njia nane kuanzia Kimara –Kibaha unaendelea kwa kasi kubwa kama inavyoonekana pichani katika maeneo ya Kimara, Mbezi na Kibamba hivyo kuanza kupunguza msongamano mkubwa wa magari katika barabara hiyo ya Morogoro. 
Barabara ya Bagamoyo ambayo inaendelea kufanyiwa upanuzi
Barabara zilizoboreshwa kwenye makazi ya wakazi wa maeneo yasiyopimwa jijini Dar es Salaam. (PICHA NA IKULU).
Katika kukuza na kuenea kwa  Lugha ya Kiswahili duniani yatupasa kushirikiana kwa pamoja kuhakikisha lugha hii adhimu inafika mbali.

Serikali imejidhatiti kueneza lugha ya Kiswahili duniani ikiwemo na kuifanya kuwa lugha rasmi kwenye nchi za Ukanda wa Kusini mwa Jangwa La Sahara (SADC).

Watanzania wameaswa kutumia fursa wanazozipata kufundisha Lugha ya kiswahili kwa wageni wa mataifa mbalimbali ili kukieneza kwa kasi pamoja na kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini.

Akiwa katika majukumu yake ya kikazi, Askari polisi wa Tanzania anaeshiriki ulinzi wa Amani katika nchi ya kidemokrasia ya Congo Ally Babu, amekuwa akitumia muda wa ziada baada ya kazi kuitangaza nchi ya Tanzania na vivutio vyake vya utalii. 

Katika kuunga mkono juhudi za serikali katika kukuza lugha ya kiswahili na amekuwa akifundisha walinzi wa amani wenzake kutoka nchi mbalimbali duniani lugha ya kiswahili na wamekuwa wakivutiwa kujifunza kwa wingi.

Babu katika kuutangaza Utalii na vivutio vyake anatumia lugha za kiingereza na Kifaransa kwani wengi wa walinzi wa amani hutoka nchi mbalimbali duniani na kuwatafsiria kwa Kiswahili.

Babu anatumia fursa hiyo kwani ni njia moja wapo ya kuitangaza Tanzania na ujumbe kufika pembe zote za dunia. 

Katika kufanikisha harakati hizo za kukuza na kueneza Lugha ya Kiswahili  na kutangaza Vivutio vya Utalii, Babu amechapisha picha za maeneo mbalimbali ya utalii kama Ngorongoro, Serengeti, Kilimanjaro na Zanzibar.

Maeneo hayo yamekuwa kivutio kwa wageni wengi, na akiwaelezea kwa upana zaidi ili kuwavutia wageni kutembelea vivutio hivyo vya Tanzania. 

Tayari wageni wengine wameshaanza kuthibitisha kufika nchini Tanzania kwaajili ya utalii na familia zao.
Askari polisi wa Tanzania anaeshiriki ulinzi wa Amani katika nchi ya kidemokrasia ya Congo Ally Babu akifundisha lugha ta kiswahili kwa walinzi wa amani wenzake kutoka nchi mbalimbali duniani.