Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, jana wakati akitangaza rasmi kuzindua Tamasha la 'Tulia Traditional Dances Festival 2018' linalofanyika kila mwaka Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya, pamoja na kuwashukuru wadhamini waliofanikisha Tamasha lililofanyika Mwezi Septemba mwaka huu Tukuyu. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa Utamaduni, Lilly Beleko, aliyemwakilisha Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo (kulia) ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Air Tanzania, Ladislaus Matindi. Picha na Muhidin Sufiani
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: