Mgeni rasmi, Mratibu wa watoa huduma ngazi ya jamii mkoa wa Mwanza, Bi. Esperance Makuza,aliyemwakilisha Mratibu wa Ukimwi mkoa wa Mwanza akifungua warsha ya siku tatu ya watu wanaoishi na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi mkoa wa Mwanza katika ukumbi wa JB Belmont Hotel jijini Mwanza Jumanne Novemba 28,2017.
Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa jamii AGPAHI mkoa wa Mwanza, Cecilia Yona akielezea historia ya shirika la AGPAHI na shughuli zinazofanywa na shirika hilo nchini Tanzania.
Washiriki wa warsha hiyo wakifuatilia mada iliyokuwa inatolewa.
Mwezeshaji Gladness Olotu akiendelea kutoa mada ukumbini.
Washiriki wa warsha hiyo wakiigiza namna ya kutoa ushauri nasaha kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog.

Shirika la Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative (AGPAHI) linalojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) na UKIMWI limetoa warsha kwa Waviu Washauri kutoka mkoa wa Mwanza ili kuwajengea uwezo kwa ajili ya kuboresha huduma katika vituo vya tiba na matunzo (CTC).

Warsha hiyo ya siku tatu iliyoanza siku ya Jumanne Novemba 28,2017 katika ukumbi wa JB Belmont Hotel jijini Mwanza imekutanisha WAVIU washauri kutoka halmashauri za wilaya za Ilemela, Kwimba, Magu, Buchosa, Misungwi, Sengerema na Nyamagana.

Waviu washauri ni watu wanaoishi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi na wamejiweka wazi na huru kuwashauri watu wanaoishi na VVU katika nyanja mbalimbali ikiwemo ufuasi mzuri wa dawa, kutoa ushauri nasaha kwa wenzao,kujitolea kufuatilia na kufundisha kwa njia ya ushuhuda wa maisha sambamba na kuhamasisha Waviu kujiunga katika vikundi ili kusaidiana na kupunguza unyanyapaa.

Akizungumza wakati wa kufungua semina hiyo,Mgeni rasmi ambaye ni Mratibu wa watoa huduma ngazi ya jamii mkoa wa Mwanza Bi Esperance Makuza,(aliyemwakilisha Mratibu wa Ukimwi mkoa wa Mwanza, alisema Waviu Washauri wanayo nafasi kubwa ya kuboresha huduma za afya kwenye vituo vya tiba na matunzo.

“Nyinyi ni viungo muhimu sana katika kuwaunganisha wateja na vituo vya kutoa huduma za tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na VVU,hivyo mafunzo haya yatawafanya mpate ujuzi na uzoefu mzuri katika kuwahudumia wateja”,alieleza.

Naye Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa jamii AGPAHI mkoa wa Mwanza, Cecilia Yona alisema shirika hilo linafanya kazi zaidi kwenye vituo vya huduma na limekuwa likijuhusisha zaidi na watoto.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: