Gari dogo likiwa limeharibika
Basi la Taqwa
Watu wawili wamefariki baada baada ya gari ndogo aina ya Toyota Land Cruiser yenye namba za usajili za T862 DJW kugongana uso kwa uso na basi la Taqwa la Kampala katika eneo la Kideka, Wilayani Ikungi mkoani Singida.

Kaimu Kamanda Jeshi la Polisi, Mkoa wa Singida,Isaya Mbughi amesema ajali ambayo imetokea Ikungi mkoani humo leo Jumamosi Novemba 11, 2017.

Amesema miili ya abiria hao wa ambao majina yao wala makazi yao bado hayajulikana, imehifadhiwa katika hospitali ya misioni Puma.

Kamanda Mbughi amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa kuna kila dalili dereva wa gari ndogo alikuwa amelala na gari lilihama kutoka upande wa kushoto,na kwenda kulia.

“Dereva wa basi amejitahidi mno kukwepa gari hilo ndogo,lakini ilishindikana na hivyo kuingia uvunguni mwa basi.Kwa wakati huo, lilihama upande wake wa kulia na kwenda nje ya barabara, lakini alilifuata huko huko”, amesema.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: