(Katikati) ni mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Geita, Leornad Kiganga Bugomola,akifuatiwa (kulia) na Mkurugenzi wa halmashauri hiyo,Mhandisi Modest Aporinal pamoja na makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Costantine Molandi wakati wa kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo.
Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Geita, Leornad Kiganga Bugomola akielezea tatizo la mfanyabiashara wa nyama ambaye amekuwa akipigwa na wafanyabiashara wenzake.
Baadhi ya madiwani wakiwa kwenye kikao hicho.
Mkuu wa wilaya ya Geita, Mwl. Herman Kapufi akisisitiza wafanyabiashara kutokubuguziwa na mtu yoyote kwenye shughuli zao wakati wa kikao hicho cha baraza.
Diwani wa kata ya Kalangalala, Sospeter Mahushi akichangia swala la wafanyabiashara.
Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Geita pamoja na mkurugenzi wakijadili jambo wakati wa kikao cha baraza la madiwani.
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Geita,Barnabas Mhoja Mapande akizungumza na madiwani wakati wa kikao hicho.

Serikali Wilayani Geita imesema kuwa mfanyabiashara anayehitaji kuwekeza kwenye biashara ya kuuza nyama kwa bei nafuu anaruhusiwa kufanya biashara hiyo sawa na watu wengine bila ya kubughudhiwa na mtu ama kikundi chochote.

Hatua hiyo imekuja kutokana na mfanyabiashara ambaye jina lake halijafahamika mara moja kufungua duka la nyama na kuuza kwa Sh,3500 kwa kilo kuambiwa na umoja wa wamiliki wa maduka ya nyama kuwa afunge kwa kuwa wao wamekuwa wakiuza kwa Sh 6,000 kwa kilo moja.

Amedaiwa kuwa anauza nyama kwa bei ambayo haijazoeleka mjini Geita na kwamba bei hiyo imezoeleka kwenye Kata ya Kasamwa.

Akizungumza wakati wa baraza la madiwani wa halmashauri ya Mji wa Geita,Mwenyekiti wa halmashauri ya hiyo Bw, Leornad Bugomola alisema kumekuwa na kikundi kinachopanga bei ya nyama mjini humo na hivyo kusababisha kumtoa mwekezaji aliyekuwa akiuza nyama kwa bei ya chini.

“Mkuu wa wilaya kutokana na watu kuhangaika kufuata nyama Kasamwa sisi tulionelea tumuombe mtu aje afungue Bucha ambayo itakuwa na Bei nafuu hivyo alikubali lakini kimezuka kikundi ambacho kimekuwa kikimpinga muwekezaji huyu na kwamba afunge bucha yake kutokana na wao kutokuafiki bei hiyo ili swala nimeona nikwambie ili uweze kulishughulikia”Alisema Bugomola

Kutokana na maombi hayo mkuu wa wilaya ya Geita, Mwl.  Herman Kapufi alisema katika wilaya anayoiongoza anataka kitu bora na kwamba suala la bei haliwezi kuwafanya watu kutowekeza kwenye wilaya yake na kama kuna watu wengine ambao wanauza bei nafuu ya nyama ni vyema wakapatiwa maeneo ya biashara hiyo kwani hakuna mtu ambaye anaweza kuingilia biashara ya mtu mwingine.

Baadhi ya wakazi wa mjini Geita wamepongeza uamuzi huo wa serikali kwa kuwa wengi hawana uwezo wa kumudu bei ya nyama ya sasa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: