Mabaki ya ndege ya shirika la Coastal Aviation iliyokuwa ikitoka uwanja wa ndege wa kia kuelekea Seronera kwenye mbuga ya Serengeti.
ZOEZI la kuokoa miili ya abiria na rubani waliopata ajali wakiwa kwenye ndege shirika la Coastal Aviation iliyoanguka eneo la bonde ya Mpakai wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha limefanikiwa kwa kuipata miili yote 11 na kuipelekea hospitali ya Mount Meru kwa ajili ya taratibu nyengine za kutambuliwa na mazishi.

Ndege hiyo iliyoanguka majira ya saa saba mchana, kutokana na matatizo la hali ya hewa ya mvua na wingu zito iliyosababisa kupoteza mwelekeo na kuanguka na kuua abiria 11 waliokuwa ndani ya ndege hiyo.

Ndege hiyo ya shirika la Coastal Aviation iliokuwa ikitokea Mkoani Kilimanjaro kuelekea eneo Seronera katika mbuga ya Serengeti ikiwa na abiria wa watanzania sita (6) na raia wa kigeni watano (5) ambao wote walifariki dunia.

Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la tukio, Kaimu Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro Theresia Mahongo amesema zoezi la kutafuta miili hiyo limekwenda vizuri japokuwa lilikuwa ni gumu kutokana na korongo ndege ilipoangukia na kwa sasa taratibu nyengine za utambuzi wa miili hiyo utaendelea.

Mahongo amesema mpaka sasa tayari miili yote imepatikana na tutaipelekea wilayani Karatu na baadae mkoani Arusha lakini pia niwashukuru wananchi wa eneo hili kwa ushirikiano mkubwa walioutoa katika kufanikisha zoezi hili.

Kwa upande wake, Naibu Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro, Dkt Maurus Msuha amesema wamejitahidi na kufanikiwa kuipata miili ya marehemu wote wa ajali na kuiondoa katika eneo la tukio kwa ushirikiano wa wenyeji wa eneo hilo pamoja na askari wa hifadhi ya Ngorongoro.

Pia Msuha amesema askari wa Hifadhi ya Ngorongoro wamelala katika eneo la tukio pamoja na wenyeji kwa lengo la kuhakikisha miili hailiwe na wanyama ambao wanapatakana ndani ya hifadhi, jambo ambalo limesaidia kuweza kuikuta miili hiyo ikiwa salama “Alisema Dkt.  Msuha.

Runda Moller ni mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo amesema zoezi hilo lilikuwa gumu kutokana na eneo ambalo ajali hiyo ilipotokea kuwepo kwa korongo kubwa ambalo lina msitu mnene na hivyo kuwafanya wao kushindwa kufika kiurahisi.

Moller amesema wakati wa ukoaji wa miili hii umekuwa mgumu na umechukua muda mrefu kutokana na korongo kuwa kubwa liniurefu wa zaidi ya mita 3,000 kutoka usawa wa bahari pamoja na msitu mnene wenye wanyama wakali na hali ya ukungu kutawala eneo hilo lakini tumefanikisha tunamshukuru Mungu.

Naye Leak Thomas ambaye ni miongoni mwa mashuhuda wa ajali hiyo amesema kabla ya ndege hiyo kuanguka ilikuwa ikizunguka kwenye korongo hilo kwa muda wa zaidi ya robo saa bila kuruka kwenda kwenye maeneo mengine mpaka ilipoanguka.

Thomas amesema wakati nikiwa katika shughuli zangu za kawaida ghafla niliona ndege ikiwa angani lakini baadae ya muda kidogo niliona inazunguka yenyewe ikiwa kwenye eneo la korongo imepoteza mwelekeo na baadae ya muda kuanguka chini. Mwisho
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: