Rais Jumuiya ya Wafanyabishara wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo nchini Tanzania, Mukendi Kabobu akizungumza na waandishi wa habari juu ya hatua ya kuondolewa kwa vikwazo vya kibiashara katika bandari ya Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jumuiya ya Wafanyabishara wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo nchini Tanzania, John Kapeta akizungumza na waandishi habari juu ya urahisi wa kupata huduma katika bandari ya Dar es Salaam pale wanapotaka kuotoa mizigo mkutano ulifanyika jijjini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya jamii.

Jumuiya ya wafanyabiaashara wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo waishio nchini Tanzania wameeleza kuridhishwa na mazingira ya ufanyaji wa biashara nchini ukiligansha na ilivyokua awali ambapo ilikua na changamoto mbalimbali.

Wakizungumza na waandishi kwa kutatua changamoto walizozilalamikia ikiwemo Urasimu wa utoaji wa mazigo bandarini ,Wamesema hapo nyuma kulikuwa na urasimu ulisababisha idadi kubwa ya wafanyabiashara wanaotoka nchini Kongo kukacha kutumia bandari ya Dar es salaam.

Rais wa Jumuiya ya Wafanyabishara Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo nchini Tanzania, Mukendi kabobu, amesema wanaipongeza serikali ya Tanzania kupitia kwa Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa kuondoa vikwazo vya kibiashara katika uondoshaji wa mizigo katika bandari ya Dar es Salaam.

Amesema kuwa wafanyabiashara wa Kongo kila wakiwa na mambo ambayo yamekuwa kikwazo kwao yamekuwa yakitatuliwa na kufanya biashara kuwa nyepesi katika kupitishia bandari ya Dar es Salaam.

Makamu wa Rais Jumuiya hiyo, John Kapeta amesema kuwa wa wafanyabiashara wanaotoka nchi ya Kongo wanafanya biashara bila kikwazo kutokana na jitihada alizochukua Rais Dkt. John Pombe Magufuli juu ya uboreshaji wa huduma katika bandari ya Dar es Salaam.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: