Wafanyakazi wa Tigo walioshiriki katika mbio ndefu za Tigo Dodoma Half Marathon wakiwa na bango linalosema 'Tumekusoma' kabla ya kuanza kwa mbio hizo ndefu jijini Dodoma leo. Tumekusoma ni kampeni mpya ya Tigo inayolenga kuwapa wateja wake urahisi wa kutumia huduma za simu pamoja na faida zaidi za bonasi kila watakapotumia namba mpya ya *147*00# kununua muda wa maongezi, bando, data na kufanya miamala ya fedha.
Mshindi wa mbio ndefu za Tigo Dodoma Half Marathon, Dickson Marwa akimaliza mbio hizo zilizofanyika mjini Dodoma hapo jana.
Baadhi ya waheshimiwa wabunge wa bunge la Jamhuri ya Mungano wa Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na medali na vyeti walivyotunukiwa kwa kushiriki mbio ndefu za Tigo Dodoma Half Marathon zilizofanyika katika jiji la Dodoma jana.
Naongoza kwa mfano na vitendo. Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dr Hamisi Kigwangala akimalizia mbio ndefu za Tigo Dodoma Half Marathon zilizofanyika katika jiji la Dodoma jana. Mhe Dr. Kigwangala alishiriki katika mbio za kilometa 21.
Mshindi wa mbio za Tigo Dodoma Half Marathon (wanaume), Dickson Allan wa Mara akipokea zawadi zake za ushindi kutoka kwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Juliana SHoza baada ya kumalizika kwa mbio hizo jijino Dodoma jana.
Mshindi wa mbio za Tigo Dodoma Half Marathon, Dickson Allan wa Mara akipngezwa na Meneja wa Tigo Kanda ya Kaskazini, Aidan Komba baada ya kumalizika kwa mbio hizo jijini Dodoma jana.
Mshindi wa mbio za Tigo Dodoma Half Marathon kwa wanawake, Noela Remi Khaday akipokea medali kutoka kwa Mkurugenzi wa Tigo, Kanda ya Kaskazini, Henry Kinabo baada ya kumalizika kwa mbio hizo jijini Dodoma jana.
Mshindi wa mbio za Tigo Dodoma Half Marathon kwa wanawake, Noela Remi Khaday akipokea zawadi zake kutoka kwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Juliana Shoza baada ya kumalizika kwa mbio hizo jijini Dodoma jana.
Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Mhe. Vumilia Nyamoga akimtunuku Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Juliana Shoza zawadi ya medali baada ya kushiriki mbio ndefu za Tigo Dodoma Half-Marathon zilizofanyika katika mji wa Dodoma jana.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: