Meneja wa Mawasiliano wa Tatu Mzuka Sebastian Maganga akizungumza mbele ya  Waandishi wa habari (hawapo pichani) mapema leo jijini Dar,alipokuwa  akimtangaza Mshindi wa milioni 60 za jackpot ya Tatumzuka. Bi Catherine Triphone (pichani kulia).
Mshindi wa milioni 60 za jackpot ya Tatumzuka. Bi Catherine Triphone (pichani kulia).akitoa ufafanuzi namna alivyoshinda hizo milioni 60 na  namna atakavyozitumia,ambapo Catherine amesema kuwa fedha hizo  atazitumia kujielimisha.
Meneja wa Mawasiliano wa Tatu Mzuka Sebastian Maganga akimkabidhi mfano wa hundi,Mshindi wa milioni 60 za jackpot ya Tatumzuka. Bi Catherine Triphone (pichani kulia).

Catherine Triphone wiki iliyopita alitimiza ndoto yake ya kusoma baada ya kushinda milioni 60 za jackpot ya Tatumzuka. Bi Catherine ambaye anaishi na wazazi wake, siku ya jumapili alikuwa nyumbani peke yake huku akisinzia alipopigiwa simu iliyobadilisha maisha yake.

Dada huyo mwenye umri wa miaka 25, amekuwa akicheza Tatumzuka mara kwa mara kwa kutumia namba zinazoendana matukio mbalimbali yanayohusu maisha yake na ndugu zake ambapo ameshinda mara kadhaa katika droo za kila saa.

"Namba zangu daima zimekuwa 842. Hizi namba zinawakilisha siku , mwezi na mwaka wangu wa kuzaliwa. Ninaishukuru Tatu Mzuka kwa kutoa fursa hii ambapo mtu yoyote anaweza kucheza na kushinda, " aliongeza Bi Catherine

Dhamira ya Tatu Mzuka kwa sasa ni zaidi ya kubadilisha maisha ya washindi wetu; tumejizatiti pia kuunga mkono mipango mbalimbali ya serikali katika jamii ili kuboresha maisha ya Watanzania wote. Mpango huu ni sehemu ya kauli mbiu yetu ya ‘Ukishinda, Tanzania inashinda’.

"Kwa ushirikiano na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Mhe. Kisare Makori tumeamua kununua vitabu kwa baadhi ya shule Wilayani humo. Tunatarajia kukamilisha taratibu zote na kutoa vitabu hivyo hivi karibuni. “ Alisema Sebastian Maganga, Meneja wa Mawasiliano wa Tatu Mzuka.

Kwa kuupendezesha msimu huu wa sikukuu, Tatu Mzuka imeahidi kufungua msimu huu wa furaha kwa kutoa shilingi milioni 500 kuanzia sasa mpaka Desemba 31, 2017. Utajisikiaje kama utamaliza mwaka kwa kupata ushindi mkubwa? Endelea kucheza, uendelee kushinda. Natumai Bi Catherine atafurahia sana sikukuu ambapo ni baada ya kucheza Tatumzuka kwa shilingi 500 tu.” Bwana Maganga alihitimisha

Bi Catherine anapanga kurudi shule kusoma kusoma shahada na kuwanunulia wazazi wake usafiri ili kuwaondolea adha ya usafiri wanayokumbana nayo. 
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: