Mshindi wa Tigo Fiesta Supa Nyota toka mkoa Morogoro, Salum Munga akiimba kwenye kinyang'anyiro cha kumpata mwakilishi wa mkoa Morogoro
Majaji wakiendelea na majukumu yao.
Mchujo wa washiriki.
Mshindi wa Tigo Fiesta Supa Nyota toka mkoa Morogoro, Salum Munga akipongezwa na washiriki wenzake.

MSHINDI wa shindano la kuibua vipaji la Tigo Fiesta Supa Nyota, mkoa wa Morogoro, Salum Munga, ametamba kuibuka na ushindi katika fainali za mwaka huu.

Kinda huyo jana aliibuka kidedea baada ya kuwapiku washiriki 106 chipukuzi waliojitojeza kuwania nafasi hiyo.

Washindi wa mashindano ya Tigo Supa Nyota kutoka mikoa 15 ya Tanzania watashindana kwenye fainali itakayofanyika Dar es Salaam mwezi huu ili kupata mshindi wa jumla.

Mshindi wa Tigo Supa Nyota, atapata nafasi ya kuendelezwa kimuziki ikiwa ni pamoja na kuingia studio.

Mara baada ya kushinda, Munga. alisema, amepata nafasi, atahakikisha anaifanyia kazi vyema na kuwapa furaha mashabiki wake wa mkoa wa Morogoro.

Alisema anejipanga vyema kuhakikisha analeta taji la Tigo Fiesta Supa Nyota kwa mara ya kwanza na kuweka historia.

Alisema anatambua kuwa ataenda kupambana na wasanii kutoka mikoa mbalimbali lakini atahakikisha anafanya vizuri na kutengeneza historia mpya.

Meneja wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo, Kanda ya kati, John Tungaraza, alisema kuwa lengo lao ni kuhakikisha wanaibua vipaji na kuwapatia daraja wasanii chipukizi kupata nafasi ya kufikia malengo.

"Tutahakikisha vijana wanafikia malengo kwani Tigo kwa udhamini wetu tunaibua wasanii chipukizi ili kuwaendeleza na kufikia malengo, kwani hatutawapa nafasi wasanii wa nje", alisema.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: