Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdalla Ulega akimsikiliza kwa makini mmiliki wa Jan's Aqua Centre Johnson Noni anayejishughulisha na ufugaji wa samaki aina ya sato katika kijiji cha Kisayanu kata ya Mbezi Wilaya ya Mkuranga, ikiwa ni katika ziara ya naibu waziri.
Mmiliki wa eneo hilo linalopatikana katika kata ya Kisayani lijulikanalo
kama Jan'S Aqua Centre , Johnson Noni amesema za ufugaji huo wa samaki
aina ya sati kuwa ni kubwa sana hasa katika upatikanaji wa chakula cha
samaki kwa sababu ya kodi kuwa juu.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdalla Ulega akikagua baadhi ya maeneo ya ufugaji wa samaki aina ya sato yanayomilikiwa na Johnsona Noni.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdalla Ulega akikabidhi mifuko ya Saruji kwa wanakijiji wa Miyekela kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa jengo la Zahanati.

Naibu Waziri wa Mifugo na Ujenzi Abdalla Ulega akisalimiana na wakina mama wa kijiji cha Mwanzenga wakati wa ziara yake katika kata ya Mbezi wilaya ya Mkuranga.
Picha zote na Emmanuel Masaka, Globu ya Jamii. Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdalla Ulega amefanya ziara katika vijiji vinne vya kata ya Mbezi na kufurahishwa na hatua kubwa waliyofikia kwenye ujenzi wa zahanati za kijiji sambamba na bwawa la Samaki lenye uwezo wa kutengeneza vifaranga milioni 2 kwa mwezi mmoja.

Akiwa katika ziara hiyo, Naibu Waziri Ulega aliweza kufahamu namna utotoshaji wa mayai ya samaki unavyofanyika ikiwemo changamoto wanazokutana nazo wafugaji wa samaki hao.

Ulega amesema, mpaka sasa kuna maeneo makubwa matatu nchini yanayofanya utotoshaji wa vifaranga ambapo kwa mkoa wa Dar es Salaam na Pwani ni Mkuranga pekee  ila kuna Kibirizi Kigoma, Naliendele Mtwara na Kinguruwira Morogoro na amechukua changamoto ya kodi ya ongezeko la thamani  kama suala la kwanza kabisa na kama wizara watalisamia kwa ukubwa wake.

Noni amedai kuwa, samaki  wanatumia sana Vyakula vya Protein ambapo ni dagaa, soya ila ukiangalia  vyakula hvyo viko juu sana ingawa serikali wametoa kodi katika mbegu za  soya ila virutubisho vinavyotengenezea chakula cha mifugo bado kipo juu.

Ameeleza kuwa uwezo wa bwawa lake linaweza kutoa vifaranga milioni mbili kwa  mwezi kwa ajili ya kuviuza kwa watu wengine wanaotaka kufuga samaki na  zaidi pia wana uwezo wa kuacha samaki wakue na kuwauza kwa wateja kwa  ajili ya kitoweo.

Kwenye Ziara hiyo, Naibu Waziri alitembelea  kijiji cha Ngalambe, Mwazenga na Miyekela na kujionea namba ujenzi wa  Zahanati za vijiji hivyo zimefikia katika hatua gani ya ujenzi pamoja na kuwapatia fedha na mifuko ya saruji.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: