Waziri wa Katiba na Sheria Prof.Palamagamba Kabudi wa pili kushoto akizungumza na ugeni wa Naibu Waziri wa Sheria wa China mhe. Zhao Dacheng katika ukumbi wa mikutano jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Sheria wa China mhe. Zhao Dacheng watatu toka kulia na ujumbe wake wakiwa katika ukumbi wa mikutano jijini Dar es salaam.
Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Kabudi aliekaa katikati akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Sheria wa China mhe. Zhao Dacheng wa pili kushoto wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza mazungumzo yao jijini Dar es salaam.

Tanzania na China wamekubaliana kuimarisha ushirikiano katika maeneo mbalimbali kama njia mojawapo ya kupambana na uhalifu wa kimataifa ambao umekuwa ukiisumbua dunia.

Makubaliano hayo yamefikiwa baada ya kufanyika mazungumzo kati ya Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi na mgeni wake Naibu Waziri wa China mhe. Zhao Dacheng ambae yuko nchini kwa ziara ya siku nne nchini.

Akizungumza baada ya kukamilika kwa mazungumzo hayo, Prof.Kabudi ameyataja makosa ya kimataifa ambayo wamekubaliana kuwa ni makosa ya kimtandao,utakatishaji fedha, usafirishaji binadamu na mengineyo ambayo yamekuwa yakiikabili dunia kwa wakati huu.

Prof.Kabudi pia amesema kwamba wamekubaliana kuimarisha ushirikiano kayika eneo la msaada wa kisheria kwa watu wenye uhitaji ambapo China pia watajifunza kutoka kwa Tanzania katika eneo hilo ambalo Inataka kuwa na sheria yake kama ilivyofanya Tanzania.

Viongozi hao pia wamekubaliana kushirikiana katika eneo la mafunzo ili kuwaongea ujuzi na uwezo watendaji wao kupitia semina za kimataifa au mafunzo maalum ili kubadilidhsna uwezo na uzoefu katika eneo la usimamizi wa sheria nchini. Tanzania na China pia wamekubaliana kushirikiana katika eneo la Mahakama ikiwa ni pamoja na usimamizi na uendeshaji wa Magereza nchini.

Awali akizungumza katika kikao hicho Naibu Waziri wa China Mhe. Dacheng alisema Tanzania ni moja ya nchi marafiki wa dhati wa China urafiki ambao uliasisiwa na viongozi waandamizi wa nchi hizo. Alisema ziara yao nchini inafungua milango mipya ya ushirikiano baina ya China na Tanzania na kuongeza kuwa itazidi kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizo.

Amesema anaamini kuwa Wizara yake imedhamiria kuisaidia Tanzania katika sekta ya Sheria ili isonge mbele kama ilivyofanikiwa China na kuongeza kuwa wao pia wataitumia nafasi hiyo kujifunzakati maeneo ambayo Tanzania imepiga hatua kama eneo la msaada wa sheria kwa watu wake.

Naibu Waziri huyo wa Sheria wa China yuko nchini kwa mwaliko wa Waziri wa Katiba na Sheria wa Tanzania Prof. Kabudi, anatarajiwa kutembelea Shule Kuu ya Sheria ya Chio Kikuu chabDar es salaam na Chama cha Wanasheria Tanganyika na Desemba Mosi ataelekea visiwani Zanzibar ambako atakutana na Jaji Mkuu wa Tanzania na viongozi wengine wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: