Rais wa Chama Cha PRST, Loth Makuza akizungumza jambo.
Meza kuu ilivyoonekana. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nicolaus William, kulia ni Rais wa Chama Cha PRST, Loth Makuza na kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Jonas Kamaleki.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nicolaus William (Kushoto) akimkabidhi cheti cha Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamini Mkapa kwa Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Jonas Kamaleki (kulia), kutokana na mchango wake wa kuagiza idara za serikali kuwa na msemaji.
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo.
Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya, Suzan Mbise aliyekuwa mmoja wa wageni waalikwa akizungumza jambo.
Wakiwa katika picha ya pamoja.

Chama Cha Maofisa Uhusiano wa Umma (PRST) kimezinduliwa jijini Dar es Salaam, ambapo maudhui makubwa ya kuundwa kwa umoja huo ni kutambulika rasmi kama taasisi na kupanuana mawazo ya utumishi miongoni mwa wanachama, ikiwa ni pamaoja na kuendesha shughuli zao kwa utaratibu maalum.

Akihutubia katika uzinduzi huo, mgeni rasmi ambaye ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nicolaus William aliwasisitizia wanachama juu ya kudumisha maadili ya umma katika utumishi wao huku akitilia mkazo suala la kujali misingi ya taaluma na matakwa ya sheria katika kulitumikia taifa.

“Nawaomba mtambue kuwa kupitia ummoja wenu huu ninyi mmebeba dhamana kubwa ya kuhakikisha mnatumika ipasavyo kwa wananchi, kwa hiyo cha muhimu ni kuzingatia maadili na misingi ya taaluma yenu ikiwa ni pamoja na kufuata sheria inataka nini, vinginevyo niwatakieni utumishi mwema katika nafasi hizi muhimu kwa jamii,” alisema.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: