Chama Cha Mapinduzi (CCM) tawi la Alimaua-A kata ya Kijitonyama- Kinondoni kimetangaza rasmi kumpokea na kumpa kadi ya uwanachama Ndg Said Mtulia aliyekua Mbunge wa Kinondoni kwa tiketi ya CUF.

Hafla hiyo fupi iliyoandalia na uongozi wa CCM tawini hapo wakiongozwa na mwenyekiti Ndg Kassim Sultani Ngonwe, Katibu Ndg Juma Mkorogo Juma na katibu mwenezi Bi Emily Sanga. Pia uongozi wa tawi uliwaalika uongozi wa Kata ya Kijitonyama na wilaya ya Kinondoni.

Katika Hafla hiyo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM) tawi la Alimaua A aliendesha zoezi la kumkabidhi kadi na hii ni mara baada ya Ndg Said Mtulia kukamilisha utaratibu wa kuomba uanachama kama ilivyooneshwa katika fungu la 9 & 10 katika katiba ya CCM, ikiwa ni pamoja na kupeleka maombi ya uwanachama na Halmashauri kuu ya Tawi kuketi kumjadili mienendo na nidhamu yake. Baada ya vikao kuridhia leo zoezi la kumkabidhi kadi likafanyika kwa kiapo cha ahadi tisa za mwanaCCM.

Katibu wa tawi hilo la Alimaua-A wa Chama Cha Mapinduzi Ndg Juma Mkorogo Juma akitoa neno katika hafla hiyo alisema" hii iwe fundisho kwa wale wote wanaohitaji kua wanachama wa Chama Cha Mapinduzi, kua ni lazima maombi yapelekwe katika matawi na CCM inauongozi nchi nzima", alisisitiza kwa kuwataka wale wote waonarudi CCM kwa njia ya mitandao kua watafute vyama vingine, CCM inautaratibu na imejengwa kwa Misingi ya nidhamu alisema.

Ndg Said Mtulia akitoa neno la shukrani alisema" anajisikia faraja kua hata msaidizi wa mjumbe wa shina ila sio kua mbunge wa Chama cha upinzani kwa kua wabunge wa vyama hivo hawawasaidii watanzania ila wanawapotosha watanzania, hilo kwake ni dhambi na ametubu kwa kujiunga na CCM". Alisema pia anajisikia ni mwenye amani zaidi alipopokelewa barua yake ya maombi katika tawi la CCM analoishi, hivyo amefarijika sana".

Huu ni mwendelezo wa wimbi kubwa la wanachama, mashabiki na viongozi wa vyama mbalimbali vya upinzani kujiunga na Chama Cha Mapinduzi katika kipindi hiki cha serikali ya awamu ya tano na baada ya mageuzi makubwa yanayofanywa na Chama Cha Mapinduzi(CCM), "kukifanya kua chama cha wanachama kinachoshughulika na shida za watu", chini ya mwenyekiti na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Ndg John Pombe Joseph Magufuli.

Imeandaliwa na;
Tawi la Alimaua- A Kijitonyama,

Imetolewa na;

Idara ya Itikadi na Uenezi
CHAMA CHA MAPINDUZI.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: