Msafara wa Magari ya waombolezaji na lililobeba mwili wa marehemu Humphrey Makundi ukipita eneo la Marangu mtoni wakati ukitoka Hospitali ya Rufaa ya KCMC kuelekea kanisa la KKKT Usharika wa Mamba Kwa Makundi wilaya ya Moshi.
Ibada ya kumuombea marehemu Humphrey Makundi imefanyika katika kanisa la KKKT Usharika wa Kwa Makundi .
Ndugu, Jamaa na Marafiki wakipita mbele ya jeneza kutoa Heshima zao za mwisho katka kanisa la KKKT Usharika wa Kwa Makundi.
Mbunge wa jimbo la Vunjo,James Mbatia akitoa heshima za mwisho katika ibada ya marehemu Humphrey Makundi.
Ndugu wakitoa heshima za mwisho.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira (wa pili toka kulia) akiwa na viongozi wengine wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wa Kilimanjaro akiwemo kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Hami Issah (wa pili toka kushoto) wakishiriki ibada hiyo.
Mbunge wa jimbo la Vunjo ,James Mbatia akizungumza wakati wa ibada ya mazishi ya marehemu Humphrey Makundi.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Anna Mghwira akizungumza wakati wa ibada ya mazishi ya marehemu Humphrey Makundi.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akimfariji Baba mzazi wa Humphrey,Bw Jackson Makundi.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Anna Mghwira akimfariji ,Mama mzazi wa Humphrey ,Bi Joyce Makundi.
Msaidizi wa Askofu ,Mchungaji Elingaya Saria akizungumza wakati wa ibada hiyo.
Baadhi ya Ndugu wa Marehemu wakifuatilia ibada hiyo.
Ndugu wa Marehemu wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa marehemu Humphrey Makundi wakati ukipelekwa nyumbani kwao kwa ajili ya kuupumzisha katika nyumba yake ya milele.
Baba mzazi wa Humphrey akilia kwa uchungu wakati jeneza lenye mwili wa mwanae likiingizwa nyumbani kwao kijiji cha Mamba kwa Makundi wilaya ya Moshi .
Mama mzazi wa marehemu Humphrey Makundi ,Bi Joyce Makundi akilia kwa uchungu wakati jeneza lenye mwili wa mwanae lilipofikishwa nyumbani kwao kijiji cha Mamba kwa Makundi.
Jeneza lenye mwili wa marehemu ,Humphrey Makundi likiingizwa kaburini .
Wadogo wa marehemu Humphrey wkiweka shada la maua katika kaburi.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira akiweka shada la maua katika kaburi la Humphrey Makundi.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, akijiandaa kuweka shada la maua katika kaburi la marehemu Humphrey.
Mbunge wa jimbo la Vunjo, James Mbatia kaiweka shada la maua katika kaburi la marehemu Humphrey Makundi.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: