Mojawapo ya washindi 35 wa zawadi za kila siku za shilingi milioni moja na shilingi laki tano katika promosheni inayoendelea ya 'Tumia Tigo Pesa na Ushinde', Prochess Mroso (kulia) mkaazi wa Kimara Temboni jijini Dar es Salaam akielezea kuhusu ushindi wake katika mkutano na waandishi wa habari leo. Ameambatana na Meneja wa Wateja wa Tigo Pesa, Mary Rutta (kati) na mshindi mwengine Editha Malyamoto wa Kibamba(kushoto). Tigo pia inatoa zawadi kubwa za shilingi milioni 15, milioni 10 na milioni 5 kwa wateja wanaotumia Tigo Pesa. 
Mojawapo ya washindi 35 wa zawadi za kila siku za shilingi milioni moja na shilingi laki tano katika promosheni inayoendelea ya 'Tumia Tigo Pesa na Ushinde', Prochess Mroso (kulia) mkaazi wa Kimara Temboni jijini Dar es Salaam akielezea kuhusu ushindi wake katika mkutano na waandishi wa habari leo. Ameambatana na Meneja wa Wateja wa Tigo Pesa, Mary Rutta (kati) na mshindi mwengine Editha Malyamoto wa Kibamba pamoja na Afisa Mawasiliano wa Tigo, Umi Mtiro (kushoto). Tigo pia inatoa zawadi kubwa za shilingi milioni 15, milioni 10 na milioni 5 kwa wateja wanaotumia Tigo pesa. 
Baadhi ya washindi 35 wa zawadi za kila siku za shilingi milioni moja na shilingi laki tano katika promosheni inayoendelea ya 'Tumia Tigo Pesa na Ushinde wakiwa na simu zao baada ya kupokea ujumbe wa simu uliothibitisha kupokea zawadi hizo za pesa.Tigo inatoa zawadi ya shilingi milioni moja kila siku na zawadi nne za shilingi laki tano kila siku kwa wateja wanaotumia huduma ya Tigo Pesa, pamoja na zawadi kubwa za shilingi milioni 15, milioni 10 na milioni 5.
Mary Rutta, Meneja wa Wateja wa Tigo Pesa akizumgumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika hafla ya kukabidhi zawadi saba za shilingi milioni moja na zawadi 28 za shililingi laki tano kila mmoja kwa washindi wa wiki hii wa promosheni inayoendelea ya 'Tumia Tigo Pesa na Ushinde'. Kushoto ni Afisa Mawasiliano wa Tigo, Umi Mtiro. 
---
Huduma ya kutuma na kupokea fedha inayoongoza nchini Tanzania, Tigo Pesa imewaibua jumla ya mamilionea saba (7) wapya katika droo ya wiki hii ya promosheni yake inayoendelea ya ‘Tumia Tigo Pesa na Ushinde’. 


Washindi wengine 28 nao wamejinyakulia donge nono za kila siku za TZS 500,000 kila mmoja, na kufanya jumla ya wateja walipotakana hadi sasa kufikia 90. Akitangaza washindi wa wiki hii katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Meneja wa Wateja wa Tigo Pesa, Mary Rutta alisema kuwa pamoja na zawadi hizo za kila siku, wateja wa Tigo Pesa wana fursa kubwa ya kushinda zawadi kubwa za TZS 15 milioni, TZS 10 milioni na TZS 5 milioni ambapo washindi watajulikana usiku wa kuamkia mwaka mpya. ‘Kufikia sasa tumtoa jumla ya TZS 69 milioni kwa washindi 90 na bado tuna zawadi za TZS 51 milioni zitakazotolewa kwa washindi wengine 63, ikiwa pamoja na mamilionea wapya tutakaowapata usiku wa kuamkia mwaka mpya wa 2018. Kushiriki katika promosheni hii ni rahisi na ni wazi kwa wateja wote wa Tigo Pesa. Kadri unavyotumia huduma ya Tigo Pesa ndivyo unavyojiongezea nafasi ya kushinda, kwa hiyo nawaasa wateja wote wa Tigo wachangamkie fursa hii ya kutimiza ndoto zao za sikukuu na mwaka mpya’ alisema. Tigo Pesa inajivunia kufanya miamala ya zaidi ya TZS 1.7bn kila mwezi kupitia mtandao wake mpana wa mawakala zaidi ya 70,000 waliosambaa nchini kote.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: