Miaka hii ya Teknolojia na mawasiliano nilitegemea gharama za internet / data kuwa chini zaidi, Ila cha kushangaza ISP / Hawa wanaotoa huduma ya internet wanaongeza gharama zaidi wanapoona watu wanatumia data sana.

Hii mnakosea sana ISP mlitakiwa kupunguza gharama za internet kadri watu tunavyoongezeka kutumia internet, wekeni faida kiduchu kwenye data wakati huohuo mapato yenu yataongezeka kutokana watumiaji wa data kuwa wengine zaidi.

Mikonga ya fiber iko kibao kuna ule Wa SEACOM na ule wa taifa NICTBB Ila cha kushangaza bado data zinapanda tu deile badala zishuke na watu tuko wengi tunaishi kwa internet.

Punguzeni gharama za internet kila mtu ana smartphone sasa na pia ili kwenye internet cafe wasiweke matangazo ya kusema huruhusiwi kuchek YouTube au kudownload, maana Mimi nimeenda kuchek YouTube hapo internet badala ya kuweka bando ambao mngefaidi ISP, Ila mkiweka bando afodabo kwa mfano kwa TZS. 500 napata 1GB kwa mwezi basi Wa bongo wote tutahamia mtandao wako.

CC: Airtel Tanzania
Vodacom Tanzania
TTCL Tanzania
Halotel Tanzania
Tigo Tanzania

Imeandikwa na Mdau Raymond BillGates Maganga.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: