Watanzani hili suala la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) linaleta ukakasi kwa sababu sehemu Fulani lazima tukubali, serikali ilitoka kwenye njia yake kuhusu Shirika la Nyumba la Taifa, na hapa anatafutwa mchawi, atakaye kamatwa kama mchawi anaweza kweli kuwa ameloga (ameloga) au asiwe mlozi lakini kabebeshwa mgomba uliokuwa unaanguka ili awe ndiye aliyeusukuma kuanguka!

1. Tujiulize, function roles za NHC ilipokuwa inaanzishwa ni zipi, na lini zilibadilika, zilipobadilika focus zake zilikuwa nini? Je, wananchi wanazijua kwa maana wawakilishi wa wananchi katika bunge letu tukufu wanajua hili, na mabadiliko yake wanayajua?

2. Kama NHC ilikuwa imetoka kwenye njia yake, ni kwa nini waheshimiwa sana wabunge walikuwa wamenyamaza hadi Rais wetu ndiye aje kuliona hilo? Kama hivyo ndivyo NHC ilikuwa inatakiwa kufanya, bunge litachukuwa hatua gani, kwa uamuzi wa Waziri kuuvunja uongozi mzima wa shirika bila sababu ya msingi?

3. Ni vizuri watanzania tukajua Shirika la Nyumba la Taifa lilipounganishwa na Msajiri wa nyumba, zilitengenezwa focus gani kwa malengo yale yaliyokuwepo katika kila shirika kabla ya kuunganishwa?

Kwa mtazamo wangu, Mkurugenzi wa NHC asihukumiwe kwa jinsi alivyo liendesha Shirika, kwa sababu haiwezekani hata kidogo kwa Shirika la uma lililo chini ya uangalizi wa wizara liendeshwe na kufanya kazi zake kinyume na sera ya wizara na serikali, hapa Mkurugenzi huyu atakuwa anaonewa, kama kweli kuwajibishwa kwake ni jinsi alivyo liongoza shirika, aliyepaswa kuwajibika wa kwanza ni Waziri, kwa nini Waziri na wasaidizi wake wote hawakuona uozo huo hadi Rais aone na ndipo wao wachukuwe hatua?

Maoni yangu, na haya ni maoni tu, Mkurugenzi kama katenda kwa ubadhirifu kwa lengo la kujinufaisha yeye ni kweli anastahili kuwajibishwa, lakini wasiwasi unaojitokeza, matendo haya ya kujinufaisha yametendeka kwa mwezi huu wa au miezi miwili iliyopita? Kama ni kwa kipindi chote cha utendaji na uongozi wake, ni kwa nini hatua za kumuondoa kwenye madaraka zifanyike leo na siyo tangu alipoanza? Ina maana nchi hii haina vyombo vya serikali vyenye uwezo wa kubaini makosa pindi pale yanapoanza kutendeka, vyombo hivyo vinabaini makossa pale tu Rais wa nchi anapo yaona au kutaarifiwa na vyombo vyake vya usalama?

HAPA KUNA SIRI ILIYOJIFICHA AMA LIPO TATIZO KUBWA KULIKO HILI TUNALO AMINISHWA.

Imeandikwa na Lazaro Kadili.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: