Msanii Irene Uwoya aliyeleta gumzo.

Na Kajunason/MMG.

Msanii wa Bongo Movie ameleta gumzo kwenye mtandao ya jamii baada ya kumsifia msanii mwenzake Irene Uwoya kwa kusema kuwa, "Happy Birthday Mwanamke mzuri kuliko wanawake wote bongo movie... Huu ndiyo ukweli msanisamhe,"

Kauli hiyo imepokelewa vibaya na baadhi ya wasanii wenzake ambao wameanza kumshambulia kwa kumtukana matusi.

Ujumbe wake huu hapa:-

shamsaford: Yaani jana kusema huyu mwanamke ni mzuri kuliko wanawake wote wa bongo movie imekuwa shida.Yaani mpaka mnanitumia msg za matusi?

Binadamu nyinyi ni watu wa ajabu sana aisee... Huu ndo ukweli mbishe na mkatae kwa upande wangu na nyinyi wote mnaokubali moyoni halafu machoni mnakataa huyu ndo mzuri.

Hana kasoro hata moja kwa vitu vya muonekano... Amejaaliwa na Mwenyezi Mungu kuanzia juu mpaka chini. Mimi huwa nalionaga kama lijini... Mbaya zaidi ni mzuri na ana mvuto akipita lazima akusitue... Maana kuna wengine wazuri lakini hawana mvuto wakipita kama hajapita mtu.

Wanawake kusifiana ni ngumu ila Mimi niko tofauti huwa siwezi kuacha kumsifia mtu pale anapofanya jambo zuri au ana vitu ambavyo huwezi acha kumsifia. Narudia tena IRENE ni mwanamke mzuri mwenye mvuto kuliko wanawake wote wa bongo movie hadi wanamziki amewafunika, ingekuwa enzi zile angeshindana na dada yangu Ray C maana ndiyo mwanamziki wa kike ninaeonaga ana mvuto na mzuri.

WANAWAKE TUNA ROHO MBAYA SANA MAANA YANAYONITUKANA DM NI WANAWAKE.ENDELEENI KUNITUKANA LAKINI UKWELI NDIYO HUO.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: