Naibu Waziriri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na Vijana, Anthony Mavunde (wakwanza toka kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi, Masha Mshomba (wa pili toka kushoto) ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa Baraza za Wafanyakazi mapema leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziriri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na Vijana, Anthony Mavunde (kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi, Masha Mshomba (kulia) wakionyesha rasmu ya Baraza la Wafanyakazi wa Mfuko wa WCF.

NA K-VIS BLOG, FELIX ANDREW

Waajiri Tanzania Bara wametakiwa kuwashirikisha wafanyakazi wao kabla ya kufanya maamuzi mbali mbali ili kuendelea kudumisha amani na mshikamano maeneo ya kazi.

Ushauri huo ulitolewa jjini Dar es Salaam jana na Naibu Waziriri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na Vijana, Anthony Mavunde, wakati akizindua baraza la wafanyakazi wa mfuko wa fidia kwa wafanyakazi (WFC)

Alisema kuwa uongozi shirikishi na wa pamoja ndiyo njia pekee itakayopunguza migogoro maeneo ya kazi, hivyo waajiri hawana budi kuhakikisha jambo hilo linazingatiwa ipasavyo.

“Lengo kuu la uongozi shirikishi na wa pamoja ni kujadiliana changamoto mbali mbali na kuzitatua kwa nia ya kufikia malengo,” alisema.

Mavunde aliwaasa wafanyakazi nchini kuondokana na urasimu katika kutoa huduma mbali mbali kwa jamii.

“Urasimu katika utoaji wa huduma ni changamoto kubwa sana ambayo inaisumbua nchi naomba sana msifanye hivyo kwa manufaa ya taifa letu,” alisema.

Aidha naibu waziri huyo alisisitiza kwa waajiri wasio jiunga na Mfuko huo kufanya hivyo mara moja kabla sheria haijachukua mkondo wake
Wafanyakazi wa mfuko wa fidia kwa wafanyakazi (WFC) wakifurahia uzinduzi huo.

Alisema kuwa serikali itaanzisha msako mkali mwakani wenye lengo la kuwakamata na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria waajiri wote ambao bado hawajajisajili na mfuko huo.

Aliongeza kuwa serikali ilikwisha toa muda wa kujisajili kwa wasiofanya hivyo ambao ulimalizika tarehe 30 Septemba mwaka huu.

Mnamo mwezi Januari mwakani tutaanzisha msako wa kuwasaka na kuwafikisha kwenye vyombo vya dola waajiri wote ambao wameshindwa kujisajili na mfuko hadi sasa, alisema

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi la WCF Bw Masha Mshomba, alisema kuwa kwa kutambua umuhimu wa kuwashirikisha wafanyakazi katika maamuzi mbali mbali ya kiutendaji tayari menejimenti kwa kushirikiana na tawi la chama cha wafanyakazi wa serikali na afya (TUGHE) imekamilisha uundaji wa baraza hilo.

Aliongeza kwa mfuko huo umeendelea kutimiza majukumu yake katika kuchangia maendeleo ya taifa, husani uchumi wa viwanda kwa kuendelea kuwahudumia wafanyakazi wanoumia au kuugua kutokana na kazi kwa nia ya kuwawezesha kurudi kazini.

Aidha mfuko pia unashiriki moja kwa moja katika kujenga uchumi wa viwanda kwa njia ya ubia na Mifuko mingine ya hifadhi ya jamii nchini.

Katika kusogeza huduma jirani na wadau wote , alisema mfuko umepanga kufungua ofisi zake katika mikoa minne katika robo ya tatu ya mwaka 2017/18.

Aliitaja mikoa hiyo kuwa ni Dodoma, Arusha , Mwanza na Mbeya huku lengo likiwa ni kuwa na ofisi katika mikoa ishirini.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: