Mapenzi ya kweli yanazidi kutokomea siku hadi siku kufuatia jinsi ambavyo matukio ya usaliti yamekuwa yakiongezeka kwenye Ndoa  na Mahusiano ya kawaida. Ni tukio la kweli ambalo lilitokea hapa jijini Dar es salaam - Buguruni - Rozana,- mitaa ya Mivinjeni ambapo kijana mmoja ambaye alikuwa na Mke aliondoka asubuhi bila kuacha kodi ya meza kwa Mkewe kwa madai kuwa hana pesa hata kidogo.

Baada ya kijana hutyo kuondoka vizuri kabisa nyumbani huku akipewa moyo wa ufanisi na Mkewe, aliondoka na kuaga kuwa anaelekea kazini, hivyo hakumuachia Mke hela ya kula, hali kadhalika ndani hakukuwa na kitu chochote cha kula.

Chaajabu kijana huyo baada ya kutoka  alielekea kwenye Mgahawa ambapo walikuwa wanauza Supu, kisha akaagiza na kuanza kula bila ya kujali Mkewe amemuacha katika mazingira gani, Mungu mkubwa Mke alijiongeza akapata wazo la kwenda kukopa vitu gengeni ili Mumewake akirudi akute chakula.

Mke akiwa anaelekea gengeni muda mfupi baada ya Mume kutoka nyumbani alimfuma Mumewake akila Supu wakati nyumbani alimwambia kuwa hana hela hata shilingi mia. Kilicho jili tafadhali tazama Video hii iliyo chezwa kama Filamu fupi yenye mafunzo baada ya kushuhudia tukio live.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: